Breaking News

RAIS DK. SHEIN ASHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KWENYE ENEO LA NYUMBA ZA WAZEE, SEBULENI ZANZIBAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika Nyumba za Wazee Sebleni Unguja, kushoto ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico
 BAADHI ya Vijana wanaoshiriki katika zoezi la Usafi wa Mazingira katika eneo la Sebleni Nyumba za Wazee wakifanya usafi
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Vifaa vya Usafi Katibu wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi A Unguja Farida Juma, kwa ajili ya zoezi la Usafi katika Wilaya yao, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Nyumba za Wazee Sebleni wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Usafi
 VIJANA wa Mabaraza ya Vijana ya Mkoa wa Mjini Magharibi na Wananchi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa usafi wa mazingira katika eneo la Nyumba za Wazee Sebleni, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Usafi wa Mazingira katika viwanja vya Sebleni Unguja.(Picha na Ikulu

No comments