Breaking News

RC MTWARA AWAHIMIZA WANANCHI WA WILAYA YA MASASI KUPANDA ZAO LA MHOGOMkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akipanda mchhe wa muhogo katika zoezi la kupanda ,iche ya zao hili katika shamba la shule ya msingi Chisegu.
=================

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewahimiza wananchi wa wilaya ya Masasi kupanda zao la mhogo ili waweze kujiongezea chakula na kipato kutokana na zao hilo kuwa na soko kwa sasa.

Hayo ameyasema Leo aliposhiriki zoezi la kupanda mihogo katika shamba la shule ya Msingi Chisegu kijijini Chisegu Wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Mheshimiwa Byakanwa ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Oktoba 26 mwaka jana amekuwa na kampeini kubwa ya kuhamasisha kilimo cha zao hilo ambalo ni zao kuu la chakula mkoani hapa. Lengo la hamasa hiyo ni kuepukana na njaa, pia njia mbadala ya kujiongezea kipato.

Licha ya hamasa ya zao la mhogo Mheshimiwa Byakanwa amekuwa akiwasisitiza wananchi kulima zao la Korosho kama zao la biashara ambapo ameitaka Bodi ya Korosho pamoja na wadau wote wa kilimo kuhakikisha wanajiandaa ipasavyo kuondoa changamoto zote za uzalishaji wa mazao mkoani Mtwara.

Aidha amewataka vijana kujiunga katika vikundi vya kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo mihogo kwani mbegu za kisasa zinapatikana
 No comments