Breaking News

MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA LEOWAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa  Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mwamboya (kushoto akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba, wakati), wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU),  kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi, mjini Unguja, jana. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando (kushoto), akikabidhidhi msaada wa viti vya wagonjwa na vifaa vingine vyenye thamani ya sh. milioni 10  kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa, kuadhimisha miaka 13 ya mamlaka hiyo, hospitalini hapo, Dar es salaam, jana.SAFINA Mohammed (kushoto) anayedai kuzaa na raia wa China Zhou Qin ambaye alifukuzwa nchini, akiwa na mtoto wake akisubiri kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kueleza changamoto anazopata  baada ya kutelekezwa na mwenza huyo, janaNo comments