Breaking News

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

MKUU wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Mchungaji Philipo Majuja (kushoto), akipokea kitabu cha Kuran Tukufu kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee. Anayeshuhudia kushoto wa kwanza ni Mchungaji wa Kanisa la Bwiru, Ephafra zabron na kulia ni Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya ziwa Hashimu Ramadhan. 


WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philemon Mpango, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB – Sehemu ya Mashariki, Gabriel Negatu, Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani wakijadiliana jambo baada ya kikao, juzi, mjini Dodoma, juzi.


MENEJA wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (KOJ), Captain Paul Paul, (kushoto) akitoa maelezo kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, kuhusu kazi za mita za kupimia mafuta, Dar es Salaam, jana.


WAZIRI wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, akifungua jengo jipya la kuhifadhia dawa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja, jana, ambalo limejengwa kwa msaada wa Mfuko wa dunia Global Fund Support  


MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia), akimkabidhi dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo mkoani hapo, 
No comments