Breaking News

NAMNA KABICHI INAVYOTIBU SARATANI

Namna kabichi inavyotibu saratani, kupoteza kumbukumbu na kukatika nywele

NA MWANDISHI WETU

KABICHI ni mboga yenye umbo la duara inayofanywa na majani mapana.
Majani hayo ni laini yenye rangi ya kijani mpauko au meupe kwa ndani, ambapo mara nyingi kwa juu huwa na rangi ya kijani iliyokolea.

Kabichi ni mboga maarufu na inatumika kote duniani, huandaliwa kwa namna tofauti lakini zaidi huchemshwa ama kuliwa mbichi katika mchanganyiko ujulikanao kama kachumbari.
Kabichi ina manufaa kwa kuwa inao uwezo wa kutibu magonjwa kadhaa ikiwemo ya ngozi, vidonda vya tumbo, kufunga choo, maumivu ya kichwa, unene kupita kiasi, mapunye, maumivu ya magoti, mifupa na mishipa.


Magonjwa mengine ni ya moyo, saratani, homa ya manjano na katika ubongo hususan kupoteza kumbukumbu, fizi zinazotoa damu.

Kabichi ni kinga dhidi ya magonjwa katika mfumo wa upumuaji ikiwemo kifua na mafua, pia inasaidia kupona haraka kwa majeraha mwilini na kukarabati tishu zilizoharibika. 

Kabichi hufanya kazi vema kwa kuponya magonjwa hayo iwapo itatumiwa kila mara, kwani inabeba virutubishi vinavyoongeza kinga ya mwili, hivyo ni muhimu kwa watoto na wazee, katika kupambana na maradhi.

Kabichi imesheheni vitamini C kwa kiasi kikubwa kuliko machungwa ambayo husifika kuwa na vitamin hiyo kwa kiwango cha juu.

Vitamin C, ni miongoni mwa virutubishi vilivyosheheni viini vinavyozuia chembe haribifu zinazosababisha magonjwa mwilini, pia hupunguza hali ya mwili kuchoka, jambo linalosababisha kuzeeka haraka.

Pia husaidia kuimarisha na kukarabati mwili, hivyo kabichi ni lishe yenye msaada kwa maisha ya binadamu.
Hata hivyo kabichi imesheheni nyuzinyuzi ambazo huuwezesha mwili kutunza maji na kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula, hivyo huusaidia mwili dhidi ya uzito uliopitiliza.
Ukosefu wa nyuzinyuzi mwilini ambao husababisha mtu kokosa haja kubwa, ndiyo chanzo cha magonjwa ya vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kukosa hamu ya chakula na saratani katika tumbo la chakula.
Pia hali ya mwili kukosa nyuzinyuzi ndiyo chanzo cha kuzeeka haraka, magonjwa kadhaa hususan ya ngozi.

Pia kabichi ina madini ya salfa ambayo huusaidia mwili kupambana na maambukizi ya bakteria, hususan yatokanayo na majeraha.

Pia salfa inasaidia kupunguza maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo, pindi mgonjwa anapoanza kutumia kabichi.

Kabichi inaelezwa kuwa ni zao lenye faida, hufanya maajabu mwilini na  linalopatikana kwa wingi na  kwa gharama nafuu.

KUZUIA SARATANI
Kabichi ipo katika kundi la    brassica ikiwemo spinachi, ambapo pia inajulikana kama mbogamboga zenye viini lishe vyenye nguvu ya kuzuia uharibifu wa seli mwilini.

Hivyo viini lishe vinavyopatikana kwenye kabichi na aina zingine za mboga jamii hiyo, hutafuta seli mwilini zinazoweza kuwa na madhara kwa afya na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuleta magonjwa ya moyo na saratani.

Kabichi ina kompaundi zinazoitwa ‘lupeol’, ‘sinigrin’, na ‘salforafen, zinazoukinga mwili dhidi ya saratani.

Kompaundi hizo huchochea kazi ya vimeng’enyo na kupunguza ukuaji wa uvimbe ambambe husababisha saratani.

Utafiti wa matumizi ya kila mara ya kabichi na mboga mboga za jamii yake ulifanywa kwa mwanamke wa Uchina, ambapo matokeo yalionyesha kuponya kwa kasi saratani ya matiti iliyokuwa inamkabili.

KUZUIA UVIMBE

Pia kabichi inajulikana kama kinga dhidi ya uvimbe na maumivu makali, kutokana na majani yake kuwa na kiambata kinachoitwa ‘glutamaini’.

Kiambata hicho kina nguvu kubwa ambayo huifanya kabichi kupuunguza madhara ya uvimbe, kuungua, maumivu ikimemo ya maungio, mzio, homa na magonjwa ya ngozi.


KUSAIDIA UONI

 Kabichi hupata umaarufu kwa watu wenye umri mkubwa hususan wazee, kwa kuwa huitumia kuzuia macho kuptoona kutokana na  kiambata kinachoitwa ‘beta karotini’ kilichomo ndani yake kinachosaidia uoni.

Si kuzuia kupofuka tu, bali kiambata hicho kinachopatikana kwenye kabichi husaidia kukuza afya njema ya macho, na kuzuia saratani.

KUPUNGUZA UZITO

Kabichi inafaa kwa watu wanaokusudia kupungua uzito wa mwili, huku wakibaki na afya njema.
Hiyo ni kutokana na kuwa na nishati kidogo na ‘utajiri’ wa vitutubishi, ikiwemo vitamini muhimu, nyuzinyuzi na madini ya kutosha, inashauriwa kufaa kama mlo sahihi kwa anayepunguza uzito.

Hivyo, licha ya kuweza kuliwa mbichi, kabichi inaweza kuandaliwa kwa mtindo wa supu, ama kula kwa wingi majani yaliyopikwa kiasi ili kuwa na afya bora, pasipo uzito wa mwili wa ziada.

AFYA YA AKILI

Mboga hii huboresha kwa kiasi kikubwa afya ya akili na inajulikana kama ‘kichocheo cha akili’.
Hiyo ni kutokana na kuwa na vitamin K ya kutosha ikiwemo kiambata cha ‘anthosianin’ ambazo huamsha akili kwa kiasi kikubwa ikiwemo umakini.

. Vitamin K ni muhimu kwa kuwa hujenga ubongo na kuikinga mishipa isidhurike, hivyo huondoa uwezekano wa magonjwa ya akili ikiwemo kusahau. 

Hata hivyo, kabichi nyekundu, inasadikiwa kuwa na virutubishi lukuki kuliko vilivyomo kwenye ile ya kawaida.

Kabichi inayo madini ambayo hata yakiliwa kwa wingi kiasi gani hayaathiri afya ya binadamu, badala yake yanaimarisha, hivyo inashauriwa ulaji wa zao hilo kwa kiasi chochote awezacho mtu.

KUTIBU MIFUPA
Kabichi ikitumika kila mara pamoja na mboga za zingine za jamii hiyo, husaidia kukinga na kuponya mifupa kwenye  mwili awa binadamu.

Hiyo ni kutokana kuhodhi madini aina ya kalsiam, magniziam na potasiam kwa wingi, ambayo ni kinga dhidi ya mifupa.


SHINIKIZO LA DAMU
Kutokana na uwepo wa patasiam ndani yake, kabichi inao uwezo wa kurekebisha shinikizo la damu hususan la juu ambalo husababisha shambulio la moyo na hatimaye kupooza.

Pia patasiam iliyomo katika kabichi, ikiliawa hufanyika msaada kwenye mishipa ya damu kwa kuwa huifungiua na kufanya damu itembee ipasavyo mwilini.

Inashauriwa kabichi kutumiwa na watu wenye msongo wa mawazo, ili mishipa inayoingiza na kutoa damu kwenye moyo   isisinyae.

Hivyo matumizi ya mfululizo ya kabichi 
Huuepusha mwili dhidi ya hali zote za hatari.

KUTUNZA NGOZI
Kama ilivyoelezwa awali, kabichi ina virutubishi vya kutosha ambavyo husaidia kutunza seli katika mwili wa binadamu, ikiwemo vitamin C, salfa na anthosianin.

Hivyo hutumika kama chachu muhimu ya afya ya ngozi na mwili kwa jumla, hususan wakati wa utu uzima.

Vinginevyo, ni rahisi ngozi ya mwili kukunjamana, kupoteza rangi ya asili na kupata madoa, hivyo hirutubishi vinavyopatikana kwa kula kabichi huaweza kubadili mwonekano na kumwacha mtu akionekana kijana na mwenye afya njema.

KUONDOA MAUMIVU YA MISULI

Kwa kiasi kikubwa matumizi ya kabichi husaidia kuondoa maumivu ya misuli.
Aina fulani za bakteria zikikutana na sukari iliyomo kwenye kabichi, huzalisha asidi adimu aina ya laktik, ambayo kwa kiasi kikubwa huondoa uchovu na maumivu.Pia kabichi inao uwezo wa kuondoa sumu mwilini ambapo husafisha damu ambapo huondoa asidi aina ya yurik, inayosababisha maumivu katika magoti, mifupa, magonjwa ya ngozi na mapunye.

Nguvu ya kuondoa sumu katika damu inasababishwa na kiwango cha juu cha vitamin C na salfa, inayopatikana katika kabichi.

FAIDA ZINGINE

Kabichi ina madini aina ya ‘ayodin’ ambayo hudaidia ufanyaji kazi bora wa mfumo wa fahamu, ubongo na vichocheo katika mwili wa binadamu. 

Virutubishi vingine vinavyopatikana kwenye kabichi ni Vitamin E, ambayo hutunza ngozi, macho na nywele.

Kalsiam, magniziam na potasiam zinazopatikana kwenye kabichi, kwa jumla huuwezesha mwili kuwa na afya bora. Pia hutibu mishipa iliyovimba ama kusogea kutoka maeneo inapostahili kuwa na maumivu ya miguu.

FAIDA ZA KABICHI NYEKUNDU
Mara nyigi aina hii ya kabichi hupendelewa kuliwa na Wachina kwa kuchanganywa kwenye chakula ama kutiwa katika supu, au kachumbari.

Hiyo husaidia kuishi maisha yenye afya bora na marefu.
Watu wengi hupendelea kabichi iliyopikwa kwenye mlo, lakini kupika kunaondoa virutubishi muhimu ikiwemo kutomeng’enywa kwa baadhi ya vitamini ikiwemo C.

Hivyo, inashauriwa kuliwa ikiwa mbichi ili kutunza vitamini na kusaidia mmeng’enyo mwilini.

No comments