Breaking News

SAMORA TOURE;BABU WA SEKOU TOURE MMBABE ALIYEWAFURUSHA WAKOLONI

SAMORI TOURE: Mbabe wa kivita aliyewatoa jasho Wafaransa

L Ndiye babu wa Sekou Toure, aliyewafurumusha wakoloni wa Kifaransa, Guinea
NA MWANDISHI WETU
AFRIKA kuna hazina kubwa ya mashujaa waliojitolea uhai wao katika kuhakikisha wanazikomboa jamii zao dhidi ya utumwa uliokuwa ukiwazalilisha utu wao kutokana na kuuzwa kama bidhaa katika mataifa mbalimbali ya Ulaya na Marekani.

                            SAMORI Toure
Mmoja kati ya mashujaa hao ni mfalme wa mapigano ambaye zaidi ya miaka 100, aliweza kuyachachafya majeshi ya Ufaransa na kuonyesha Afrika ni bara lenye hazina kubwa ya mashujaa wapiganaji dhidi ya sera za kikandamizaji.


SAMORI TOURE NI NANI?

Samori Toure alizaliwa mwaka 1830, katika Mji wa Manyambaladugu katika Kijiji cha Kankan Kusini mwa nchi ya Guinea.


Ni miongoni mwa wapiganaji mashuhuri waliowahi kutokea katika vita dhidi ya mabeberu wa kibepari katika karne ya 19 baada ya kukataa kukabidhi himaya yake kwa wakoloni wa Ufaransa.


Akiwa na umri wa miaka 20, Samori alikuwa akijishughulisha na kufanyabiashara, lakini baada ya mama yake kutekwa na kuuzwa utumwani na Mfalme Sori Birama, aliamua kujiunga na jeshi akiwa na maana ya kujijengea nguvu, mbinu za kivita na ushawishi kwenye jamii yake.

 SAMORI Toure (mwenye nguo nyeupe) akiwa na wapiganaji wake
 Aidha, Samori alikuwa na mtazamo wa kuunganisha makabila ya Malinké ili kunza kujenga himaya yake kwa kutumia mbinu za kimila na kufanikiwa kuziunganisha tawala za kichifu za Malinke na kuwa chini ya himaya yake.

Hivyo, alifanikiwa kuzifanya jamii hizo mbili kuwa katika himaya ya umoja na kujenga jeshi imara kwenye himaya hiyo iliyotajwa kuwa kuongozwa kwa ufanisi na mtawala huyo.

Alijenga ngome iliyokuwa na nidhamu, utendaji kazi wa kisasa, uwajibikaji huku akiwapa mafunzo askari wake kupitia mbinu za kisasa kwa wakati huo kwa kutumia silaha za moto.

Jeshi lake aliligawanya majeshi yake mara mbili ambapo kundi la kwanza alilita “Sofa” lilikuwa la askari wa miguu lenye wapiganaji kati ya 30,000 na 35,000 pamoja na jeshi la maji aliloliita “Sere” likiwa na wapiganaji 3,000.

Ukizungumzia katika historia ya majeshi ya kale ya Afrika, basi jeshi hili lilikuwa imara zaidi ambapo himaya yake iliimarika kati ya mwaka 1883 na 1887, na kuipa jina la Almami na kuitawala kwa misingi ya imani ya Kiislam.

 
 Sekou Toure, Mwasisi wa Taifa la Guinea ambaye pia alikuwa mjukuu wa Samori Toure
 Baada ya himaya yake kuimarika zaidi, Samori Touré aliiita hiyo ilikuwa kati ya mwaka 1852 na 1882, huku ikijitanua zaidi maeneo ya mashariki hadi katika himaya ya Sikasso ambapo leo hii inaitwa Mali.

Himaya hiyo ilijitanua zaidi na kuhusisha mataifa ya sasa ya Guinea, Mali, Ivory Coast na Gambia.

Miaka ya 1850, ndipo biashara ya utumwa ilipigwa marufuku hivyo mataifa ya Ulaya yaliazimia kuanzisha utawala wao barani Afrika, na kuziamuru himaya zote zilizokuwa zikiongozwa na Waafrika zijisalimishe.

Lakini, hali ilikuwa ngumu kuzimaru himaya imara kama za Mandika chini ya Kiongozi wao Samori Toure.

Mwaka 1882, kutokana na uimara wa Himaya ya Mandinka, Ufaransa ilimshutumu ed Samori Touré kwa kukataa kutii amri ya kituo cha biashara cha Kenyeran baada ya majeshi yake kuweka vikwazo vya kuzuia watu kuingia katika eneo hilo.

Hivyo, Ufaransa ailitangaza vita vilivyopiganwa kuanzia mwaka 1882 hadi 1885, na kulazimika kuingia mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano mwaka 1886 na 1887.

Lakini, mwaka uliofuatia vita viliibuka upya baada ya Ufaransa kuvunja makubaliano ya kusitisha vita, lakini licha ya hivyo aliweza kuyashinda majeshi ya Ufaransa kuanzia mwaka 1885 hadi 1889.

Mwaka 1890, aliyaunganisha majeshi yake na kuingia mkataba na Uingereza waliokuwa wakiitawala Sierra Lione ambapo aliweza kujipatia siraha za kisasa na kumfanya kuongeza nguvu kwenye jeshi lake kwa kuwashambulia Wafaransa kwa mbinu za msituni.

 Disemba mwaka 1891, Majeshi ya Ufaransa yalifanya mashambulizi ya kushtukiza kwenye mji mkuu wa Mandinka na kusababisha vifo vya mamia ya wakazi huku Samori Toure akikimbia Mashariki mwa himaya hiyo.

Aliamua kuamisha makazi yake kutoka mji wa Bisandugu hadi Dabakala huku majeshi ya Ufaransa yakiamua kukusanya silaha kwenye makoloni yake ya Magharibi mwa Sudan mabayo ni Senegal, Mali na Niger kupambana na Samori.

Kati ya mwaka 1893 hadi 1898, Majeshi ya Samori yaliamua kurudi nyuma kuelekea mji ya Bandama na Como (Ivory Coast ya sasa) ambapo aliweza kuteka eneo kubwa la eneo hilo nakuharibu miumbombinu ya mji huo kuzuia kusonga mbele kwa majeshi ya Ufaransa.

 Mei 1, 1898,Majeshi ya Ufaransa yaliuteka mji wa Sikasso hivyo majeshi ya Samori yalikimbilia katika misitu ya Liberia kujipanga upya, lakini kutokana na kupigana vita kwa muda mrefu alijikuta akikosa siraha za kutosha kupambana na Ufaransa.

Alijikuta akizidiwa nguvu na kukamatwa Septemba 29, 1898, kwenye kambi yake kwenye mji wa Guelemou nakuhamishiwa nchini Gabon ambapo baada ya miaka miwili alifariki mwezi Juni mwaka 1900.

Samori Touré alikuwa mpiganaji aliyejenga umoja wa Waafrika kwa kuunda jeshi imara kuwadhibiti Wakoloni na urithi wake kumwachia mjukuu wake aliyekuja kuwa kipenzi cha Afrika Ahmed Sekou Toure aliyekuja kupigania Uhuru wa Guinea.

No comments