Breaking News

HATIMAYE KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI YA TANZANITE ONE YAKILI KOSA, YAKUBALI KUILIPA TANZANIA FIDIA, KODI. YAMMWAGIA SIFA JPM. NI BAADA YA KUUNDA TUME. SERIKALI YAAHIDI KUIPA USHIRIKIANO.ANARIPOTI MWANDISHI WETU HATIMAYE Kampuni ya kuchimba madiniya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayo kubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali, imeelezwa.
Makubaliano hayo ya metiwasain leo iJijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais, Dk. John Magufuli, Profesa Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wakamati ya majadiliano kwa upande wa Serikali, Profesa. Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa Serikali fidia kutokanana na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioipa Serikali hasara.
Alisema fidia hiyo inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo na haitahusisha kodi.
Pia, Kampuni hiyo ya Tanzanite One italazimika kulipa kodi kama kawaida inazodaiwa na Serikali na tozo nyingine zote zinazo daiwa na Serikali.
Kwa mujibu wa Kabudi, Serikali imekubaliana na Kampuni ya Tanzanite One kuwa itafuata masharti yote ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaeleza kuwa ni Watanzania tu ndiowanaoruhusiwa kuchimba madini ya Vito na endapo hawakutakuwa na uwezo, ndipo wanapoweza kuingia ubiana wageni.
Aidha,Prof. Kabudi alisema, kuhusu wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzanite katika eneo la Mirerani, utaratibu mpya unawekwa lengo kubwa likiwa ni kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inalenga madini ya vito kuwa mikononi mwa Watanzania.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Kampuniya Tanzanite One Faisal Juma, alimshukuru Rais Magufuli kwa kuunda kamati hiyo ya Kizalendo katika kufuatilia rasilimali za madini nchini ambapo wameweza kujadiliana na kufikia muafaka wa kulipa fidia ikiwa ni mbali na malipo yote yaliyotakiwa kulipwa Serikali ikiwemo kodi.
Alisema, Tanzanite One itahakikisha inafuata taratibu zote za sheria ya madini ya mwaka 2010 kwa lengo la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo hautajirudiatena.
"Sisi kama Tanzanite One tunaihakikishia Serikali kuwa uaminifu uliotuonyesha nasi si pia kama Kampuni tutahakikisha tunakuwa waaminifu na kuwa zao hil ilinanufaisha taifa kutokana na imani aliyotuonyesha Rais kama wananchi wake kutupa nafasi na fursa ya kusikilizwa ili kurekebisha makosa tuliyoyatenda", amesema   Faisal.
Faisal alisema Tanzanite One itahakikisha haitafanya makosa iliyofanya maraya kwanza na hivyo kuwa mfano wa kampuni nyingine za madini kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania.No comments