Breaking News

MATUKIO KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIPOZINDUA RASMI MRADI WA UUNGANISHWAJI UMEME WA GRIDI YA TAIFA JANA KATIKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA KWENYE KITUO CHAUMEME CHA TANESCO KILICHOPO KIJIJI CHA MAHUMBIKA MKOANI LINDI JANA.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua rasmi Mradi wa Uunganishwaji Umeme wa Gridi ya Taifa katika Mikoa  ya Lindi na Mtwara kwenye Kituo cha Umeme cha TANESCO kilichopo katika Kijiji cha Mahumbika Mkoani Lindi,jana. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
MAJALIWA akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee baadaya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ziara ya siku moja mkoani humo
 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa  akipofya katika mtando wa kompyuta wa TANESCO ili kuiunganisha mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye  Gridi ya Taifa  wakati alipozindua  rasmi Mradi wa Uunganishwaji Umeme wa Gridi ya taifa  katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye Kituo cha TANESCO kilichopo katika  Kijiji cha Mahumbika mkoani Lindi
 BAADHI ya viongozi na wananchi waliohudhuria katika sherehe ya  kuzindua rasmi Mradi wa Uunganishwaji  Umeme wa Gridi ya Taifa katika mikoa  ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha TANESCIO kilichopo katika Kijiji cha Mahumbika mkoani Lindi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani), wakati alipowahutubia baada ya kuzindua mradi huoo.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua  Mradi wa Uunganishwaji Umeme wa Gridi ya Taifa katika mikoa wa Lindi na Mtwara . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Kituo cha TANESCO kilichopo katika  kijii cha Mahumbika mkoani Lindi, kulia ni Kalemani.

No comments