Breaking News

WANANCHI WA WILAYA YA KISARAWE KUPATIWA MAJI YA UHAKIKA. NI BAADA YA KUTIWA SAINI MKATABA WA ULAZAJI BOMBA LA MAJI KUTOKA KIBAMBA HADI KISARAWE MKOANI PWANI LEO KATI YA DAWASA NA KAMPUNI YA CHINA HENAN INTERNATIONAL COOPERATION GROUP CO LTD (CHICO) YA NCHINI CHINA

 KAIMU Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi 
na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang'ingo na 
 Ofisa Mkuu wa Fedha wa China Henan International 
Cooperatio Group, Wang Xiaogang, wakitia saini mkataba wa 
mradi wa ujenzi wa ulazaji bomba la maji kutoka Kibamba hadi  Kisarawe, Mkoani Pwani, leo. Kutoka kulia ni 
Mbunge wa Kisarawe na Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na 
Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo, Waziri wa Maji na 
Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, Mkuu wa Mkoa wa 
Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo na Mbunge wa viti maalumu Zainab Vullu 
maalumu, Zainab Vulu.
NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), imetiliana saini na Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Mkataba wa ujenzi wa mradi wa kulaza bomba la maji na matenki kutoka Kibamba hadi kisarawe mkoani Pwani.
Utiawa saini kwa mkataba huo ulifanyika leo Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, kumeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mkoani humo Zainab Vullu.
Kwa mujibu wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Romanus Mwang’ingo, mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10,849,788.50.
Mwang’ingo alifafanua kuwa mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 kuanzia leo na kwamba hatua hiyo inatokana na Rais Dk. John Magufuli, hivi karibuni kuiagiza DAWASA kufanya hivyo mara moja jambo ambalo limetekekelezwa.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Kamwele alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na ukikamilika utanufaisha wakati wa wilaya hiyo.

Kamwele alisema kusukuma maji kitakachokuwa na uwezo wa kufungwa pampu nne, ununuzi na ufungaji wa pampu mbili zenye uwezo wa kusukuma maji kiasi cha lita 60 kwa sekunde kwa kima cha mita 180.
Pia kujengwa kwa kituo cha kupokea maji chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 480,000.
Hata hivyo alisema, sehemu kubwa ya vifaa vya ujenzi wa mrdi huo yakiwemo mabomba, vitanunuliwa katika viwanda vya hapa nchini ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.
Alisema hatua hiyo itachangia kwa kiasi Fulani kuimarisha uchumi wan chi na kuwataka wananchi waishio wilayani humo kuwa waaminifu katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi huo.
Mhandisi Kamwele aliwahakikishia wananchi wa hao mbele ya Mbunge wao Jafo, kuwa wizara yake itafanya kila jitihada ili kumaliza tatizo la maji katika maeneo mengine ya wilaya kabla ya kumalizika mwaka 2020 ikiw ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
“Niwahakikishie wajukuu zangu kwamba nitahakikisha maeneo mengine yenye shida ya maji katika wilaya yenu yatapata maji kabla ya mwaka 2020.
“Sasa tunafanya kazi tu kutekeleza ahadi zetu tulizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wetu. Naomba tushirikiane kuulinda mradi huu ili uweze kukamilika salama,” alisema Kamwele.
Awali akimkaribisha mgeni ramsi, Waziri Jafo alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ikikabiliana na tatizo la maji katika kipindi kirefu.
Alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa kuitupia jicho wilaya hiyo ambapo sasa itakuwa imepata maji ya uhakika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha utawala wake.
Alisema kukosekana kwa maji ya uhakika katika wilaya hiyo kumeifanya ikose maendeleo, lakini sasa si ajabu kuona ikiwa katika nafasi nzuri kiuchumi baada ya kukamilika kwa mradi huo.
“Naamini kabisa ndg yangu waziri mwenzangu Babu yetu Kamwele baada ya kukamilika kwa mradi huu wilaya yetu itakuwa na viwanda vingi na kuzalisha ajira kwa vijana wetu,” alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu Zainab Vullu alimshujkuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake aliouchukua kuiagiza DAWASA kufanikisha mradi huo.
MWANG'INGO na Xiaogang wakibadilishana hati za mikataba hiyo 
 WANANCHI wakishuhidia hafla hiyo
 KUTOKA kushoto ni Mwang'ingo, Kamwele, Jafo na viongozi wengine waliyrshuhudia kutiwa saini kwa mkataba huo

 MBUNGE wa Kisarawe, Suleiman Jafo, akisalimiana na 
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Mjitaka Dar 
es Salaam, Nelly Msuya, kabla ya hafla ya utiaji saini 

WAZIRI Kamwele akizungumza katika hafla hiyp. Kutoka kushondo ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evalist Ndikilo na Jafo
 VIONGOZI hao wakifuatilia kwa makini hafla hiyo
 MHANDISI Ndikilo akizungumza katika hafla hiyo
 WASANII wakifanya vitu vyao kusheresha hafla hiyo
 MKUU wa wilaya ya Kisarawe Hapiness Senega aakitoa nasaha zake. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalumu Zainab Vullu
 WAZIRI Jafo akiteta jambo na Mhandisi Ndikilo
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Kamwele akiteta na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'pingo wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Waziri Jafo 
JAFO akizungumza kwenye hafla hiyo

No comments