Breaking News

MAPYA YAIBULIWA NA IGP SIRRO UTEKWAJI WA ‘MO’
Na Mwandishi Wetu.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro ameibua mapya katika kikao alicho kifanya asubuhi ya leo na waandishi wa habari ikiwemo pamoja na  kuthibitisha kuwa Jeshi la polisi hali hitaji msaada juu ya matukio yanayojitokeza.

IGP amesema kuwa bado jeshi la polisi linauwezo wa kushughulika na wahalifu pamoja na vitendo vya kihalifu vinavyoendelea  kujitokeza.

“Suala la nani aje kutusaidia, sisi ndio tunajua nani aje, na tukiona kuna haja lazima tutamtaarifu Amiri Jeshi Mkuu kwamba tunafikiri hapa tusaidie, lakini kwa hali uliyonayo sidhani kama tunahitaji watu watusaidie, lazima tulinde heshima ya nchi yetu”

Hayo ameyazungumza baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Serikali imekataa msaada wa kiuchunguzi kutoka kwa mataifa ya nje.

Sirro alisema kuwa jeshi la polisi lina kesha usiku na mchana kuhakikisha linafanikisha upatikanaji Mohamed Dewji ‘Mo’.

“Niwatumie salamu Hawa wahusika wa tukio hili, Hii ni siku ya tisa tunazunguka, watu wangu hawalali,Tukiwakamata watajua Hii ni Tanzania.”

Hata hivyo alitaja baadhi ya hatua ambazo mapaka sasa uchunguzi wa polisi umebaini ikiwemo uchunguzi wa risasi iliyo okotwa na kupelekwa katika maabara zao huku pia akisema kuwa risasi hiyo inaukubwa wa milimita 9,huku  akiweka bayana kuwa wamefanikiwa kufanya utambuzi wa gari iliyo tumika kufanya tukio zima ambayo ni AGX 404 MC na gari hiyo imetokea nchi jilani.

Jeshi la polisi linaendelea na ‘operation’ nchinzim ili kuthibiti wizi wa magari na tayari magari 42 yamesha patikana na kuwalika wenye magari yao kwenda kuyachukua.

No comments