Breaking News

MBUNGE AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA DARASANI


Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattemba, ameamua kuingia darasani mwenyewe ili kupima ufahamu wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Misuna wakati alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni. Mattembe, ambaye alikuwa njiani kwenda kwenye mahafali ya wahitimu wa Kidato cha Nne katika Sekondari ya Pohama wilayani Singida, alikoalikwa kuwa mgeni rasmi.

Lakini, akiwa njiani Mattembe ambaye kitaaluma ni mwalimu, aliamua kuingia shuleni hapo ili kujiona kazi inayofanywa na walimu, kukagua miundombinu ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na walimu na wanafunzi.

Baada ya kupewa maendeleo ya shule hiyo, alikwenda kujionea mwenyewe darasani na aliridhika na kuelezea furaha yake kutokana na umahiri wa wanafunzi katika kufahamu mambo mbalimbali.

Akiwa shuleni hapo, alielezwa changamoto ya uchakavu wa baadhi ya miundombinu ambapo, alitoa msaada wa mifuko 30 ya saruji kama mkakati wa haraka wa kukabiliana na tatizo hilo huku akiahidi kurudi. Pia, ameahidi kuwa atarejea shuleni hapo kwa ajili ya majadiliano ya kuangalia njia bora ya kumaliza changamoto zinazoikabili kwa kuhusisha wadau wa maendeleo na serikali.No comments