Breaking News

TRUMP AKATAA SERIKALI YAKE KUUFICHA UKWELI JUU YA KIFO CHA KHASHOGGINa Mwandishi Wetu.
Rais wa marekani Donald Trump amekataa serikali yake kuhusishwa na kuficha ukweli juu ya kuuwawa kwa aliye kuwa mwandishi nguri wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi.Trump alizungumza hayo akipinga taarifa zilizo ihusisha serikali serikali yake na kuuficha ukweli juu ya kifo cha mwandishi huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ikulu jana.
“hapana,hata mimi nataka kujua nini kimetokea,hakuna anaye ficha ukweli na siufichi ukweli lakini tuna tegemea kupata ukweli wa tukio zima mwishoni mwa wiki hii”.Rais trump ameongeza na kusema anatarajia ripoti kamili kutoka kwa katibu mkuu Mike Pompeo baada ya kukamilika kwa kikao cha kidiplomasia kati ya Saudia pamoja na Uturuki ili kumuwezesha kufanya tathimini na kutambua nini kilitokea.

Ikumbukwe kuwa Jamal kashoggi alipotea katika mazingira ya utata alipokwenda kutembelea ubalozi wa Saudi Arabia na baadae kupatikana akiwa ameuwawa huku taarifa za kiuchukuzi zikidai kuwa aliteswa kabla ya kuuwawa.
                             

No comments