Breaking News

BALOZI SEIF: SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEA NA UTARATIBU WAKE WA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI ILI KUONA USTAWI WAO UNAIMARIKA MUDA WOTE.MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto), akimjuilia hali Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Suleiman Othman Nyanga, Nyumbani kwake mtaa wa Mpendae mjini Zanzibar jana.Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi, alisema Serikali ya Mapinduzi ya  Zazibar, bado inaendelea na utaratibu wake wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ili kuona ustawi wao unaimarika muda wote.

Balozi Seif,  aliyasema hayo wakati akimjuilia hali waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Suleiman Othman Nyanga, nyumbani kwake mtaa wa Mpendae mjini Zanzibar.

Alisema,  zipo taratibu zilizowekwa na serikali kupitia Wizara husika ya Afya Zanzibar, za kumpatia uhamisho mgonjwa ama awe kiongozi au mwananchi wa kawaida wa kupelekwa kwenye matibabu Tanzania Bara au nje ya nchi iwapo hali ya mgonjwa husika inazidi kuwa  mashakani hasa kutokana na ukosefu wa vipimo au utaalamu wa kina.

MKURUGENZI wa Tiba wa Wizara ya Afya Zanzibar Dk. Juma Mbwana (Mambi), akimpa maelezo Balozi Seif,  kuhusu taratibu zilizotumiwa na wizara yake za kumpeleka Nyanga, Nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Balozi Seif,  alimuhakikishia waziri huyo wa zamani wa Zanzibar kwamba, serikali itaendelea kumpa msaada wakati wowote pale atakapohitaji kulingana na afya yake licha ya kupangiwa kurejea tena kutatiwa matibabuni nje ya nchi mwanzoni mwakani.

 BALOZI Seif,  akiagana na watoto wa Nyanga  mara baada ya kumaliza mazungumzo na baba yao. (Picha zote na OMPR  Zanzibar).

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao pia walizungumzia hali ya soka Visiwani Zanzibar ambapo Balozi Seif, alimkumbusha Nyanga, enzi zake wakati alipokuwa mchezaji wa kutegemewa wa Timu ya Soka ya Miembeni wakati yeye akiwa golkipa machachari wa timu ya soka ya Ujamaa enzi zile.

No comments