Breaking News

DAWA YA WAKEKETAJI WATOTO WACHANGA YAJA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile  akiwa na Wasichana waliokolewa na vitendo vya ukatili  wa ukeketaji wanaopatiwa mafunzo ya ujasiliamali  na Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Mwandishi Wetu Manyara
Dawa ya wale wanaofanya vitendo vya Ukeketaji kwa watoto wadogo na ukeketaji kwa ujumla nchini inaelekea kupatikana kutokana na kukidhiri kwa vitendo vya ukeketaji vya aina hiyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizundua kituo Maalum cha kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukeketaji cha Shirika la NAFGEM kilichopo  Orkesumeti Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji kwani inaonekana wahusika wamenzisha mbinu mpya za ukeketaji baada ya watoto kupta elimu juu ya madhara ya ukeketaji na wengi wao kukimbia kufanyiwa vitendo hivyo.

Naibu Waziri Ndugulile amezitaja mbinu mpya za ukeketaji ni pamoja na kuwakeketa Watoto wachanga, kutofanya Sherehe wakati wa ukeketaji na kufanya vitendo hivyo nyakati za usiku.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali haipingi mila na desturi zilizopo katika makabila ndani ya Tanzania ila kusiwepo na mila zisizofaa ambazo zinaleta ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji.

"Vitendo hivi havikubaliki katika Tanzania ya awamu hii tuongeze nguvu katika kupambana na vitendo vya ukeketaji" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile pia amewataka viongozi wa kimila kutoa ushirikiano kwa Serikali na wadau katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na vitendo vya ukeketaji katika maeneo yao.

"Ni aibu kubwa sana kwa kukeketa na kuwaozesha watoto wadogo ambao tunawaharibia ndoto zao" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro  ameahidi kushirikiana na wadau katika kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji Wilayani humo.

"Nikuahidi Naibu Waziri tutaendelea na mapambano dhidi ya vitendo hivi hatutamuacha mtu salama " Alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Simanjiro Bw. Francis Selasini amesema Shirika lake liekuwa likiwasaidia watoto wa kike wanakimbia vitendo vya ukektaji na kuwapa elimu ya ujasilimari na kuwasomesha wale ambao hawakupayta nafasi ya kusoma na mpaka sasa wamefanikiwa kusomesha mtoto mmoja wa kike ambaye amerudi na kuanza kuwafundisha wenzake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Simanjiyo Mhandisi Zephania Chaula amesema Serikali yaWilaya imeweka nguvu kubwa katika kupambana na vitendo vya ukeketaji katika Wilaya hiyo na kuweka jitihada za kuondoka na mila zisizofaa zinazo mkandamiza mtoto wa kike.

Naye moja wa msichana aliyekimbia ukeketaji Nagalali Molell amesema avitendo vya Ukeketaji bado vinaendelea ktika maeneo ya vijijini na elimu zaidi inahitajika ili kuweza kuikomboa jamii hiyo kwani watoto wa kike wamekuwa wakikandamizwa kwa kulazimishwa kuolewa kukuketwa na kutopata elimu sawa wa watoto wa kiume.

No comments