Breaking News

HABARI KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WILAYANI RUANGWA.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akimpongeza  Niachia Kalembo, kutoka Kijiji cha Mtimbo wilayani Nachingwea, ambaye ni mmoja  wa wazazi waliojifungua katika Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa wakati alipotembelea kituo hicho, Novemba 18, 2018 .


MAJALIWA, akimkabidhi  khanga Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa, Grace Nanguka, ikiwa ni zawadi ya watumishi wote wa kituo hicho baada ya kukagua ujenzi na ukarabati wake.


 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akitazama Mtambo wa utakatishaji vifaa vya upasuaji katika Kituo cha Afya cha  Mkowe wilayani Ruangwa. WAZIRI Majaliwa, akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha Afya cha Mkowe wilayani Ruangwa  na Asia Abdallh (kushoto) wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi katika kituo hicho.


MAJALIWA , akikagua ujenzi wa Nyumba za makazi ya askari Magereza wakati alipokagua ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.


 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na walimu na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi  za wilaya ya Ruangwa  (hawapo pichani), kwenye ukumbi wa Narung'ombe, Novemba 18, 2018.  Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,  Hashim Ngandirwa.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).


MAJALIWA , akikagua ujenzi wa Gereza la wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

No comments