Breaking News

MIAKA MITATU YA JPM TARURA YALETA FURAHA KWA WANANCHI WA BUKOBA.Na Mwandishi Wetu, Bukoba

MIAKA mitatu ya Rais John Magufuli, madarakani inatajwa kuondoa adha ya wananchi waliokuwa wanatembea umbali mrefu na kutozwa gharama kubwa ya usafiri kutokana na uwepo wa miundombinu mibovu ya barabara katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Hilo, limefanikiwa chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), ambao imetengeneza barabara tatu kwa kiwango cha lami ambazo ni barabara ya shirika la nyumba hadi kilimahewa, Kahororo hadi Mugeza na barabara ya Kashura.

Akizungumza na Blog hii, wilayani hapa, mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Savera Kamugisha, alisema walikuwa wanapata shida kutumia barabara hizo hasa nyakati za mvua.

“Barabara hizi mwanzoni licha na kuwa mbaya na kutopitika nyakati zote, ilikuwa inasababisha ajali kutokana na kuwa nyembamba na hivyo,  magari mawili kushindwa kupita kwa wakati mmoja, lakini kwa sasa tuna furaha barabara hizi tunazitumia wakati wote na kupunguza gharama za usafiri,” alisema mkazi huyo.Diwani wa Kata ya Bakoba Jimmy Mwakyoma,  amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kulinda barabara zinazojengwa ili ziwe na manufaa kwao kwa muda mrefu.

“Mimi kama diwani nitahakikisha kupitia vikao vyetu tunaweka mikakati ya kusimamia  mapambano didi ya waharibifu wa barabara hizi,  tabu waliyokuwa wanapata wananchi ni kubwa, hivyo ni wajibu wetu sasa kulinda na kutunza barabara hizi ambazo zimetumia fehda nyingi hadi kukamilika kwake,”alisema diwani Mwakyoma.

Nae diwani wa Kata ya Kashai, Kabaju Muruhuda Kabaju, amewasisitiza madiwani kushirikiana na TARURA katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao ikiwemo miradi ya barabara ili kuharakisha ukamilikaji wa miradi hiyo.


Kwa upande wake meneja wa TARURA Manisoaa ya Bukoba mhandisi Andondile  Mwakitalu amesema katika manispaa hiyo TARURA ina jumla ya km 165.8 ambapo kati ya hizo kilomita 24.6 zimejengwa kwa kiwango cha lami.

“Katika mwaka huu wa fedha wa 2018/2019 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.53 ili kutekeleza miradi sita,kati ya miradi hiyo mitano tayari utekelezaji wake umeanza kasoro mradi mmoja mchakato wake umechelewa kutokana na kutopatikana kwa mkandarasi mwenye sifa,”alisema Mwakitalu.

TARURA imeanzishwa mwaka julai 2017 ikiwa na lengo la kufanya matengenezo endelevu ya gharama nafuu na kusimamia maendeleo ya Mtandao wa Barabara Vijijini na Mijini ili kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

No comments