Breaking News

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI KUTOKA UBALOZI WA AUSTRUA, LEO

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria nchini Tanzania (sehemu ya biashara), Kurt Mullauer (kushoto) katika Ofisi ya Naibu Waziri jijini Dodoma.
---
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria Nairobi-Kenya, (sehemu ya biashara), Kurt Mullauer aliyefika wizarani ili  kumweleza kuhusu  Ujumbe wa Kibiashara  kutoka Austria unaotarajiwa kuwasili nchini mwezi Januari, 2019.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Eng.Innocent Luoga na Mwakilishi wa Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Ebenezer Mollel.

Kurt Mullauer amemweleza Naibu Waziri kuwa, ujumbe huo wa kibishara utajumuisha makampuni 8 ambayo yanajishughulisha masuala ya afya, usafirishaji na nishati na utawasili  jijini Dodoma mwishoni mwa mwezi Januari kwa ajili ya kukutana na viongozi na watendaji wa Serikali.

Mullauer ameongeza kuwa, nchi hiyo imekuwa ikiunga mkono uendelezaji wa miradi ya umeme nchini na hadi sasa wameshatoa mikopo ya masharti nafuu kwa baadhi ya miradi ya umeme iliyo nje ya gridi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, aliushukuru ubalozi wa Austria kwa uamuzi waliouchukua wa kuyaleta makampuni hayo nchini ambapo Tanzania itapata fursa ya kueleza maeneo yanayohitaji uwekezaji hasa katika miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia lengo la kuwa na megawati 5000 ifikapo mwaka 2020.

Naibu Waziri pia amemweleza Mullauer kuhusu maeneo yote yanayohitaji ushirikiano na wawekezaji hasa ya uzalishaji umeme kwa kutumia maji, gesi asilia na nishati jadidifu na usambazaji umeme vijijini.

No comments