Breaking News

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA .OFISA Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Deograsius Michael (kulia), akikabidhi hati ya makabidhiano ya kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, Mhandisi David Shunu (kushoto), kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali. Anayeshuhudia ni Ofisa Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Benard Makan.


OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili aanze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma.

Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Musa Joseph, alisema ujenzi wa ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Rais, Dk. John Magufuli, ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya Nchi Dodoma.

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Musa Joseph (wa pili kushoto), akizungumza na Waataalam  wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa Jijini Dodoma

Joseph,  alifafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika Mji wa Serikali.

Aliongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha sh.  700, 000,000.  ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa, nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

KAIMU Mkurugezi wa Huduma za Ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, akiahidi kutimiza jukumu lake ili kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unakamilika kwa wakati katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa Jijini Dodoma.
Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David Shunu, aliishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale akisisitiza jambo kwa TBA ili kuhakikisha ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma unakamilika kwa wakati.
Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Peter Mabale aliitaka TBA kufanya mawasiliano haraka iwezekanavyo na ofisi yake pindi kunapotokea changamoto yoyote itakayokwamisha shughuli ya ujenzi badala ya kusubiri vikao ili kuitatua.

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Musa Joseph akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia wananchi.Makabidhiano ya kiwanja hicho yalifanyika baada ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga kusaini mkataba wa ujenzi wa ofisi hizo Novemba 22, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Dk. Magufuli, la kuhamishia Shughuli za Serikali makao makuu ya nchi Dodoma.

No comments