Breaking News

RAIS DK. JOHN MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU BABA ASKOFU EVARISTO CHENGULA WA JIMBO KUU LA MBEYA.RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, akitoa heshima  za mwisho kwa mwili wa marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula, wa Jimbo kuu la Mbeya, katika Ibada ya kumuaga iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 2018.
Na Mwandishi Wetu

RAIS wa JamhuriyaMuunganowa Tanzania Dk. John Magufuli leo Novemba 26, 2018, ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Mhashamu Askofu Evaristo Chengula, aliyefariki dunia Novemba 21, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar Es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Misa Takatifu ya kumuaga marehemu Askofu Chengula iliyoongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi Jude Thadaeus Ruwa’ichi, imefanyika katika Kanisa la Mtakatifu Imakulata lililopo Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu, Kurasini Jijini Dar Es Salaam nakuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamuya Tatu, Benjamin  Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa


 RAIS  Dk. Magufuli, akitia saini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu ya Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuaga mwili wa marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula.

Akizungumza baada ya Misa hiyo Rais Magufuli, alitoa salamu za pole kwa Maaskofu wote wa Kanisa  Katoliki, Mapadre, Watawa, Waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya na Wakatoliki wote nchini kwakuondokewa na kiongozi aliyekuwa akifany a vyema kazi yake ya kutangaza Injili.

Rais Magufuli alisema pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma za kiroho marehemu Askofu Chengula alisimamia ukweli ikiwemo kupinga hadharani ndoa na mapenzi ya jinsia moja licha ya kuwepo mashinikizo mbalimbali.

Akitoa salamu kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Makamu wa Rais wa TEC Mhashamu Askofu Flavian Kasalla alimshukuru  Rais Magufuli kwa ushirikiano alioutoa wakati wakuuguza na baada ya kifo cha Askofu Chengula na pia aliwashukuru madaktari na wauguzi, viongozi na wote waliokuwa wakimuombea kabla na baada ya kifo.

Mhashamu Askofu Evaristo Chengula amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo na baada ya Misa ya kumuaga mwili wake ulisafirishwa kwenda mkoani Mbeya kwa maziko. 

No comments