Breaking News

RC BYAKANWA AWATAKA WASANII WAJENGE CHUO CHA SANAA MKOANI MTWARA. *ASEMA KUNA MENGI MAZURI YA KUJIFUNZA


 
M KUU wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii hao jana, mkoani humo.Na Evarissty Masuha, Mtwara

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa,  amewataka wasanii nchini, kujenga Chuo cha Sanaa mkoani Mtwara kwakuwa una vipaji vingi vya sanaa, lakini hakuna chuo cha kuweza kuwaandaa kitaaluma.

Byakanwa,  aliyasema hayo jana Novemba 23, 2018 wakati alipotembelewa  na kikundi cha wasanii cha Wasafi ambacho kinatarajia kufanya tamasha la burudani leo Novemba 24, 2018 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ulioko mjini Mtwara.

Alisema,  sanaa ni ajira, sanaa ni fursa, sanaa ni nafasi ya kujikomboa kimaisha, lakini ina muda wake ambao msanii anatakiwa kujiandaa ili wakati huo ukifika awe na njia mbadala ya kuendeleza maisha yake.

BAADHI ya Wasanii hao wakifurahia jambo.

“Mtwara kuna waigizaji wengi,  wasanii wengi na watu wa Mtwara wanapenda sanaa… lakini kama Taifa,  tuna vyuo vichache sana vinavyoweza kuzalisha wasanii… tunawea kuwa na taasii ambayo tunaweza kuzalisha wasanii wengi na vipaji vingi zaidi.

“hizo ni fursa ambazo zipo. Mnaweza kuzitumia kwa fedha mnazozipata kwa kipindi hiki,” alisema mkuu huyo wa mkoa  Byakanwa.

Mkuu wa mkoa huo (kati kati), akipokea kutoka kwa msanii Diamond Platinum kwa ajili ya akina mama (hawapo pichani), ambapo kila mmoja alipata kiasi cha sh. 50,000.Byakanwa,  aliwashukuru wasanii wote wakiongozwa na msanii Nassib Abdul, maarufu kama Diamond Platinum kwa kuchagua kwenda Mtwara.

 Pia, ameshukuru kwa msaada walioutoa kwa makundi mbalibmlai katika jamiii ambao ni pikipiki tatu ambazo walieelekeza ziende kwa shule tatu zinazofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa, milioni tano ambazo zilimetolewa kwa akina mama 100 ambapo kila mmoja alikabidhiwa sh. 50,000, sare za shule pea 100 kwa wanafunzi 100 pamoja na madaftari, peni, penseli pamoja na vitabu.

BYAKANWA akisalimiana na mama mzazi wa msanii Diamond, ambaye jina lake halikupatikana.

Akizungumzia msaada huo walioutoa,  msanii Diamond Pratinum,  aliushukuru uongozi wa mkoa wa Mtwara kwa mapokezi mazuri waliyoyapata.

 Alisema msaada huo ni kutokana na kuguswa na hali duni ya maisha kwa jamii ya Kitanzania na kuongeza kuwa msaada huo haujatoka kwa wasafi peke yao bali ni kundi zima la wasanii waliombatana pamoja kwenda mkoani humo.

KUTOKA kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, EvodMmanda, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Byakanwa na Msanii Diamond.Kwa upande wake msanii Dudubaya,  alishukuru Serikali zote zilizotangulia na kwani yako maendeleo makubwa yaliyopatikana, lakini wengine wanajifanya hawayaoni wakati yako wazi.

 Alitolea mfano kuwa miaka ya 2005 barabara ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Mtwara,  ilikuwa ya vumbi ambapo yeye (Dudubaya), aliwahi kusafiri na alifika Mtwara,  akiwa amejaa vumbi hadi masikioni, lakini safari hii alisafiri kwa lami tangu Dar Es Salaam hadi Mtwara akiwa katika hali yake ya kawaida ya usafi.

 Alisema,  hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo kwa Tanzania.
Kikundi cha wasafi kinachojumuisha wanamuziki na waigizaji maarufu hapa nchini, kipo mkoani Mtwara,  kwa ajili  ya kufanya tamasha maalumu linalojulikana kama Wasafi Festival ambalo litafanyika leo kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kuanzia saa 12 jioni.

No comments