Breaking News

TAARIFA WANACHAMA WASIO NA DIPLOMA

WILAYA YA KASKAZINI B                                                                       14/11/2018
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI B’ MAKAME MWADINI SILIMA AMESEMA HALMASHAURI YAKE  ITAENDELEA NA JUHUDI ZA KUONGEZA VYANZO VIPYA VYA MAPATO VISIVYOKUWA MCHANGA ILI KUZIBA MIANYA YA UVUJAJI WA MAPATO  KUPITIA MACHINJIO YA DONGE MUWANDA  ,  MAHONDA ,KITALU CHA MICHE MWANAKOMBO, PAMOJA NA KITALU CHA SAKAFUNI VITAKAVYOSAIDIA KUONGEZA MAPATO YA HALMASHAURI HIYO
AMESEMA KUPITIA VYANZO HIVYO VYA MAPATO HALMASHAURI HIYO ITAWEZA KUKABILIANA NA MATATIZO  KATIKA SEKTA ZILIZOGATULIWA IKIWEMO SEKTA YA AFYA ,ELIMU PAMOJA NA KILIMO AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIIGUSA JAMII MOJA KWA MOJA KATIKA HUDUMA ZAKE.

AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA KAMATI YA KUDUMU YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA  YA BARAZA LA WAWAKILISHI  BWANA MAKAME AMESEMA NI VYEMA SERIKALI IKAFANYA UTAFITI WA KINA ILI KUONDOWA MGONGANO WA SHERIA  ZA UKUSANYAJI WA MAPATO AMBAO UNAZOROTESHA SHUGHULI ZA  UKUSANYAJI WA MAPATO KWA HALMASHAURI
HATA HIVYO AMEHAKIKISHIA KAMATI HIYO KUWA KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA MKUU WA WILAYA WATAFANYA UFATILIAJI WA MARAKWA MARA ILI KUONA FEDHA ZINAPATIKANA KWA WAKATI  ILI KWENDA SAMBAMBA NA MATARAJIO YA MAKUSANYO.

HATA HIVYO AMESEMA PAMOJA NA MIPANGO HIYO BADO HALMASHURI YAKE INAKABILIWA NA CHANGAMOTO KADHAA AMBAZO ZINAHITAJI KUTATULIWA KWA UPANDE WA ELIMU,AFYA,KILIMO NA UENDESAJI WAHALMASHAURI.
AKIZITAJA CHANGAMOTO HIZO NI  KUCHELEWA KUPATA FEDHA ZA MCHANGA PAMOJA NA KUSHUKA KWA MAPATOYATOKANAYO NA MCHNGA,UCAHACHE WA OFISI NA VITENDEA KAZI KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI,  UCHACHE NA UFINYU WA VIANZIO VYA NDANI VYA MAPATO,UCHAKAVU WA VITUO VYA AFYA,NA VITENDEA KAZI,UPUNGUFU WA WAWATUMISHI, NA UPUNGUFU WA PEMBEJEO,MATEREKTA NA DHANA NYENGINE ZA KILIMO.

AKIFAHAMISHA KUHUSIANA NA MAKUSANYO YA FEDHA KUPITIA VYANZO MBALIMBALIAMEEMA HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI  B IMEKUSANYA JUMLA YA SHILINGI MILIONI MIA NNE SITINI NA SITA LAKI SABA ELFU THEMANINI NA NNE MIA TISA NA THAMANINI NA TANO  (466,784,985 )KWA KIPINDI CHA JULY HADI SEPTEMBER 2018/2019  IKIWA NI SAWA NA ASILIMIA 93.3 YA LENGO LILOKUSUDIWA.

WAKATI HUHUO HUO NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA,SEREKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ  SHAMATA  SHAAME KHAMIS AMESEMA SEREKALI ITAHAKIKISHA  INADHIBITI UINGIZWAJI WA WANYAMA KIHOLEALA KATIKA MAENEO YA MACHINJIO KWA KUANDAA UTARATIBU MAALUM  KUPIMA AFYA ZA WANYAMA HAO ILI KUONDOWA WASIWASI WA KUPATIKANA KWA MADHARA KWA WATUMIAJI WA NYAMA NA MIFUGO.

AMESEMA KWA SASA UTARATIBU ULIOPO HAUKIDHI HAJA NA UMEKUWA UKIIKOSESHA MAPATO SEREKALI NA UNAWEZA UKASABABISHA MADHARA KWANI WANYAMA WAMEKUWA WAKIINGIZWA BILA YA UTARATIBU MAALUM IKIWEMO KUTOCHUNGUZWA AFYA ZAO.

HATA HIVYO AMESEMA PAMOJA NA KUWA BANDARI YA MUWANDA KWA SASA WANASHUSHWA WANYAMA BANDARI HIYO HAIJAWA BANDARI RASMI NATARIFA ZILIOPO BANDARI RASMI ITAKUWA NI BANDARI YA MKOKOTONI.

KAMATI YA KUDUMU YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA INAYONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE MH.MAHANO OTHMAN SAID IMEPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZILIZOFANYWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA KASKAZINI B  KWA KIPINDI CHA MIENZI MITATU YA JULY HDI SEPTEMBA MWAKA HUU.

No comments