Breaking News

TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU.


                            

.KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kushoto),   akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya mifupa (MOI), Dk. Samuel Swai,  kuhusiana na kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wakati alipoitembelea Taasisi hiyo jana Jijini Dar Es Salaam,  jana.


                                             NaWAMJW, Dae Es Salaam

TAASISI ya Mifupa (MOI), imetakiwa kuanzia jana  kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa huduma kutokuwepo mahali pa kazi ili kuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya,  wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu pamoja na vipimo.

Dk. Ulisubisya,  alisema alichokiona kwenye taasisi hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

DK. Ulisubisya, akizungumza baadhi ya wagonjwa waliofika katika taasisi hiyo kupata matibabu.

“kuanzia leo (jana), taasisi hii itawasiliana nanyi kila inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane na daktari wako muda utakaombiwa”. Alisema.

Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa wanaandika namba za simu za wateja wao.

  

Picha3.KATIBU  Mkuu Ulisubisya, akiangalia  mashine ya mionzi ya CT SCAN katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipoitembea ili kujionea hali ya utoaji wa huduma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dk. Mohamed  Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.Hata hivyo,  Dk. Ulisubisya,  alisema hii ni kutokana na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.

Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.


No comments