WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ACHARUKA *AAGIZA KUFANYIKE UCHUNGUZI FEDHA ZA KUKARABATI HOSPITALI, UJENZI KITUO CHA AFYA * NI ZAIDI YA SH. BILIONI MOJA ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI.
KASSIM MAJALIWA
Na Mwandishi Maalumu, Lindi
WAZIRI
Muu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, aunde timu
ya wataalamu kufuatilia sh. milioni 700 zilizotolewa na Serikali ili kukarabati
Hospitali ya wilaya ya Nachingwea, ambazo hadi sasa hazijatumika.
Pia, Waziri Mkuu ametaka timu hiyo ikague matumizi ya sh. milioni
400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya
Kilimarondo ambazo zimeshatumika huku ujenzi ukiwa haujakamilika.
Alitoa agizo hilo jana Novemba 17, mwaka huu, wakati akizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kilimarondo, Nachingwea, mkoani
Lindi, baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya.
“Serikali haitaki mzaha na fedha za umma, hivyo mkuu wa mkoa unda
timu ya wataalamu kutoka mkoani waje Nachingwea kufuatilia ni kwa nini fedha
zimetolewa tangu Julai ili kukarabati hospitali ya wilaya ziwe hazijatumika
hadi leo. Pia tujue kama kweli bado zipo.,” alisisitiza Majaliwa.
Agizo la Majaliwa, limekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Hassan Masala, kumueleza kwamba hadi sasa sh. milioni 700
zilizotolewa na Serikali mwezi Julai mwaka huu kwa ajili ya ukarabati wa
hospitali ya wilaya bado hazijatumika.
Mbali na fedha hizo, pia mbunge huyo alimuomba uchunguzi maalumu
ufanyike kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kilimarondo baada ya
fedha zilizotolewa kumalizika na mradi kutokamilika.
Mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya ulitengewa sh. milioni 400
ambazo zimekwisha na zinahitajika sh. milioni 51 kwa ajili ya kumalizia, ambapo
Waziri Mkuu aliiagiza halmashauri ihakikishe fedha hizo zinatolewa ili
kukamilisha mradi huo.
Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya kitakachokuwa
kinatoa huduma mbalimbali zikiwemo za mama na mtoto na upasuaji kutawapunguzia
wananchi kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 90 kutoka Kilimarondo hadi
Nachingwea kufuata huduma za afya.
Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme, Waziri
Mkuu alisema Serikali
imedhamiria kusambaza umeme katika
maeneo yote ambayo bado hayajaunganishiwa nishati hiyo nchini yataunganishiwa
ikiwemo tarafa ya Kilimarondo.
Waziri Mkuu alisema Rais Dk. John Magufuli anataka kuona kila
nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu, Serikali imetenga
fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika maeneo yote kwa gharama
ya sh. 27,000 tu.
Pia, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao kwamba hawatowajibika
tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme
kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
No comments