Breaking News

WAZIRI MKUU MAJALIWA 'AWAPASHA' WANANCHI. *AWATAKA WAWEKE PEMBENI ITIKADI ZA KISIASA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO.


 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa shule ya msingi ya kwenye kijiji cha Kilimahewa unaofanywa na wananchi  wa Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, leo Novemba 20, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Na Mwandishi Wetu, Lindi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewapongeza wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kwa kujenga shule ya msingi  kwenye Kijiji cha Kilimahewa.

“Uamuzi wa kujenga shule ya msingi ni sahihi kwa kuwa huwapunguzia watoto kutembea umbali mrefu na pia utarahisisha mazingira ya kusomea kwa watoto wetu,” alisema Majaliwa.


BAADHI ya wanawake waliojitokeza kushiriki katika ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji cha Kilimahewa  wilayani Ruangwa, wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani), wakati alipowasili kwenye eneo la ujenzi wa shule hiyo kukagua ujenzi  na kushiriki katika ujenzi huo.


Alitoa pongezi hizo leo Novemba 20, 2018, alipotembelea eneo la ujenzi wa shule ya msingi Lugalo na kuwataka waendelee na moyo huo.

Alisema, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, inataka kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule aanzishwe shule na asome.


MAJALIWA kisalimiana na viongozi wa Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa na viongozi wa Mfuko wa Human Relief Foundation wakati alipowasili kwenye msikiti huo kuuzindua

Kadhalika, Waziri Mkuu ametaka wananchi hao waweke pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake washirikiane kujenga miradi ya maendeleo kwenye eneo lao.

Nae, Mtendaji wa Kijiji cha Kilimahewa, Majuto Ungulu, alisema ujenzi wa shule hiyo uliibuliwa na wakazi wa kijiji hicho, ambacho hakina shule ya msingi.


KASSIM Majaliwa , akizungumza wakati alipozindua Msikiti wa Mbekenyera  wilayani Ruangwa uliojengwa na Mfuko wa Human Relief Foundation.

Majuto amesema watoto wa kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa kilomita mbili hadi shule la msingi Ruangwa, hivyo ujenzi huo utawawezesha kusoma karibu.

Alisema, kwa sasa wameanzia na ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 18 ya vyoo na ofisi mbili za walimu kwa gharama ya sh. milioni 399.8.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Msikiti wa Mbekenyera wilayani Ruangwa baada ya kuzindua ,

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, alitembelea kituo cha afya cha Mbekenyera  na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwataka wananchi wakitunze.

Alisema, kwa sasa wananchi hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na matibabu katika hospitali ya wilaya.


MAJALIWA, akisalimiana na Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, baada ya kuzindua msikiti huo. 

Waziri Mkuu huyo, alitaja baadhi ya huduma zitakazopatikana kwa sasa kwenye kituo hicho ambazo zamani hazikuwepo kuwa ni pamoja na upasuaji, maabara, mama na mtoto. WAZIRI Kassim Majaliwa, akiwaaga wananchi  baada ya kuzindua msikiti huo.


 Mapema Waziri Mkuu alikagua eneo la ujenzi wa kituo cha Polisi Ruangwa, alitembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya na kukagua ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya.

No comments