Breaking News

HAFLA YA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA DARAJA JIPYA NA BARABARA UNGANISHI TOKA AGA KHAN HADI COCO BEACH ILIVYOFANA.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, jana Desemba 20, 2018  aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Selander linalounganisha eneo la Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 1,030 na upana  wa meta 20.5 litakuwa na njia 4 za magari na njia 2 za watembea kwa miguu, na litajengwa pamoja na barabara unganishi zenye jumla ya kilometa 5.2.

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo zimefanyika katika eneo la Aga Khan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais,  Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mawaziri, Wabunge, Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda. 
No comments