Breaking News

KANISA KATOLIKI LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUMALIZA SAKATA LA MAFAO YA WASTAAFU.


            
RAIS Dk. John Magufuli, akisalimiana na Paroko msaidizi Padre Asis Mendokta, mara baada ya kuungana na waumini wengine katika Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. leo Desemba 30, 2018. (Picha zote na Ikulu).                          Na Mwandishi Wetu


RAIS Dk. John Magufuli, ameungana na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam kuadhimisha sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Joseph.

Misa Takatifu ya kuadhimisha sherehe hiyo imefanyika leo Desemba 30, 2018 na kuongozwa na Paroko Msaidizi, Padre Bathlomeo Bachoo, ambaye alisisitiza umuhimu wa jamii kujenga familia bora, inayochapa kazi na inayomcha Mwenyezi Mungu.
Dk. Magufuli, akisalimiana na watoto wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay.

Padre Bachoo, pia alimpongeza Rais Magufuli, kwa uamuzi wake wa kutanzua sintofahamu kuhusu mafao ya wastaafu na ametoa wito kwa familia zitakazonufaika na uamuzi huo kutumia mafao hayo kujenga umoja na kuimarisha familia zao.

Wakati huo huo, Rais Magufuli, amemjulia hali mama yake mzazi  Suzana Magufuli, ambaye anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam tangu miezi mitatu iliyopita baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (Heart Stroke).
MAGUFULI, akipeana mkono wa amani na Masista wa Kanisa Katoriki na Waumini wengine wakati wa Ibada ya leo Jumapili.

Aidha, Magufuli, aliongoza maombi ya kumuombea mama yake pamoja na watu wote wanaokabiliwa na maradhi na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2019.
RAIS Magufuli, akiwa na wasaidizi wake wakimuombea mama yake mzazi  Suzana Magufuli, anayepatiwa matibabu  Jijini Dar es Salaam leo Desemba 30, 2018. Suzana, anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa. Vilevile amewashukuru madaktari na wauguzi wanaomhudumia mama yake na wagonjwa wengine nchini na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu heri na fanaka katika majukumu yao ya kunusuru maisha ya watu.

No comments