Breaking News

KATIBU MKUU DK. TAMATAMA AWATAKA WATAALAMU WA MAGONJWA YA SAMAKI KUPAMBANA, KUZUIA MAGONJWA HAYO YANAYOVUKA MIPAKA.KATIBU Mkuu Uvuvi Dk. Rashid Tamatama (kati kati), akitoa taarifa yake fupi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wataalamu wa Magonjwa ya Samaki uliyofanyika Jijini Dar es Salaam juzi.


                              Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu Sekta ya Uvuvi Dk. Rashid Tamatama, amewataka wataalamu wa magonjwa ya samaki kupambana na kuzuia magonjwa hayo yanayovuka mipaka ( trans boundary).

Dk. Tamatama alitoa rai hiyo wakati akifungua mkutano wa  wataalamu hao wa magonjwa ya samaki  uliofanyika juzi Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulihusisha Nchi 25 duniani na wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa ajili ya ushirikiano wa nchi zote kwa pamoja ili kuweza kutambua magonjwa ya samaki yanapotokea.

Katibu Mkuu Dk. Tamatama, alieleza kuwa  nia yao ilikuwa ni kuzuia magonjwa samaki, kuyatambua ya aina gani na kuweza kuyakabili.

Alisema kuwa kwa muda wa miaka miwili iliyopita hadi kufikia June 2018, kulizalishwa tan 14,800 za samaki.

‘Tunataka mpaka kufikia mwaka 2020 tuwe tunazalisha tan 30,000,” alisema Katibu Mkuu Dk. Tamatama anayeshugulikia UVUVI.

BAADHI ya wataalamu hao kutoka nchi mbalimbali wakihudhuria mkutano huo.

Dk. Tamatama,  alisema  Tanzania ilizalisha tani laki 360 hadi 380 kwa kipindi kilichopita cha miaka 10, lakini  samak bado hawatoshelezi. 

Hata hivyo, Tamatama alisema kwamba kwa sasa wanaweka mikakati ya kuongeza samaki kwa njia ya ufugaji ili waweze kupata tani nyingi zaidi.

Katibu Mkuu huyo alisema, kwa kipindi cha mwaka tayari kuna vizimba 386,  hivyo uzalishaji wa samaki kibiashara unazidi kuongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita.

KATIBU Mkuu Uvuvi Dk. Rashid Tamatama (kulia)  akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali akiwemo Dk. Patrik Bastiaensen  (wapili kulia waliokaa), kutoka Shirika la Afya ya Wanyama (Oie) anewakilisha Afrika Mashariki.

  

Naye Dk. Hamisi Nikuli, kutoka Idara ya Uvuvi alisema sekta hiyo ni kubwa hivyo inahitaji kupatikane malighafi ambazo zitasaidia kutoa mazao ambayo yanauzika ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Dk. Kikuli, lengo la kikao hicho ni kutoa mafunzo kwa wataalamu ili kuweza kupambana na magonjwa ya samaki na viumbe vinavyo ishi kwenye maji.

No comments