Breaking News

KATIBU MKUU MALIASILI APONGEZA JUHUDI ZA KUKUSANYA MAPATO ZINAZOFANYWA NA UONGOZI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO.KATIBU Mkuu, Profesa. Adolf Mkenda, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jijini Arusha  jana,  wakati wa ziara yake (Picha zote na Nickson Nyange).

                    Na Mwandishi Wetu, Arusha

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda, ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, kwa uthubutu wake wa kutumia mifumo ya kielectronki katika ukusanyaji wa mapato.

Profesa Mkenda, alitoa kauli hiyo jana Novemba 30, 2018 alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi hiyo pamoja na wataalamu wake.

Alisema kuwa juhudi hizo pamoja na mambo mengine, zimechangia kuongezeka kwa maduhuli  na kwamba NCAA, imekuwa taasisi ya kwanza chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya maduhuli. 

Katika ziara yake hiyo ambayo ni ya kwanza ndani ya NCA tangu kuteuliwa kwake, alipokelewa na wenyeji wake Kamishna Mkuu, Dr. Freddy Manongi na Naibu Kamshina Dr. Maurus Msuha na kupatiwa maelezo mbalimbali yanayohusina na utendaji kazi wa NCAA.

Katika ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kujifunza, alikutana na uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na wataalam wa kamati maalum inayofanya tathmini  ya  sera ya matumizi mseto ya ardhi katika hifadhi hiyo.

Hata hivyo, Prosesa Mkande, aliendelea na ziara yake kwa kutembelea makumbusho mpya ya Olduvai  na ambapo amejionea mambo mbalimbali katika eneo hilo.


KATIBU Mkuu Profesa. Adolf Mkenda, akiwasili katika Ofisi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

No comments