Breaking News

MAOFISA UNUNUZI, UGAVI WATAKIWA KUTHAMINI MIRADI INAYOFANYWA NA SERIKALI.


KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Gabriel, akiwasilisha mada kwa MaOfisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani) katika Kongamano la Tisa la mwaka la maofisa hao.                                Na Edward Kondela, Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante  Gabriel, amewataka Maofisa Ununuzi na Ugavi Nchini kutambua na kuthamini miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali, kwa kuithaminisha na thamani halisi ya fedha inayotumika katika miradi.
Prof. Gabriel, aliyasema hayo jana Desemba 5. 2018  Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mada kuhusu uvumbuzi na ufanisi bora kwa Maofisa Ununuzi na Ugavi kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakati wa siku ya ufunguzi wa Kongamano la Tisa la mwaka la maofisa hao.
KATIBU Mkuu Profesa. Gabriel, akisikiliza kwa makini michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na Maofisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha mada kwa maofisa hao juu ya uvumbuzi na ufanisi bora katika masuala ya ugavi.“Katika ujenzi wa miradi mikubwa tunayoishuhudia kwa sasa nchini, fedha zinatumika, lakini jinsi gani sasa vifaa vinanunuliwa, malighafi zinanunuliwa ni jambo kubwa sana, kuna haja ya wahusika katika tasnia hii wawe wabunifu kadri iwezekanavyo na wawe ni watu wa kuleta mabadiliko,” alisema Prof. Gabriel.
Katibu Mkuu huyo aliwataka maofisa hao kuwa wavumbuzi na kufanya kazi kwa ufanisi katika masuala ya ugavi na usambazaji bidhaa ili kuisaidia serikali, kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kujenga miradi mbalimbali ili iwe na tija kwa taifa.
BAADHI ya Maafisa Ununuzi na Ugavi wakisikiliza mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante  Gabriel. (Picha zote na Edward Kondela).Aidha, Prof. Gabriel aliwataka maofisa hao, kubadili mienendo yao ambayo haiwaletei tija katika ufanisi wa kazi, pamoja na kujiongezea thamani katika jamii kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.

No comments