Breaking News

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI.


                                                    RAIS DK.  JOHN MAGUFULI

                                    Na Mwandishi Wetu
RAIS waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amemteua Jaji mstaafu. Steven Bwana, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi chamiaka mitatu.

Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Desemba 4, 2018 ilisema kuwa, Pamoja na kumteua mwenyekiti wa tume hiyo, Rais Magufuli, amewateua Makamishna  5  wa Tume ya Utumishiwa Umma.

Makamishna hao ni pamoja na George Yambesi, Balozi mstaafu. John Haule, Immaculate Ngwale, Yahaya Mbila na Balozi mstaafu. Daniel Njoolay.

Uteuzi huo wa Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma umeanza Novemba 22, 2018.

Wakati huo huo, Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amemteua Balozi Luteni Jenerali mstaafu Wyjones Kisamba, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumbu (Tanzania Automotive Technology Center).

Baloz. Kisamba anachukua nafasi ya Prof. Burton Mwamila, ambaye amemaliza muda wake.

Katika hatua nyingine, Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Mbaraka  Semwanza kuwa Kamishna wa Utawala na Fedha katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

SACP Semwanza, anachukua nafasi ya CF Michael Shija ambaye amestaafu. Uteuzi wa viongozi hao umeanza jana Desemba 4, 2018.

1 comment: