Breaking News

WATANZANIA WATAKIWA KUKUZA LUGHA YA KISWAHILI.

BALOZI  Ali Seif Iddi, (watatu kushoto), akifurahia machapisho mbali mbali ya vitabu yaliyochapishwa na Wahadhiri pamoja na watunzi wa vitabu vya kiswahili kutoka pembe zote za Dunia jana.

Na Othman Khamis Ame-OMPR – Zanzibar
MAKAMU  wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka Watanzania kufanya  jitihada ili  kuipa uhai fasihi simulizi na andishi ili  kuiepusha  hazina hiyo ya miaka mingi kupotea.
Alisema kiswahili ni lugha nzuri  inayopaswa kuendelezwa kwa kuwa  ni nyenzo ya kuchangia maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yanayokuwa  kwa kasi kubwa hivi sasa.
Akifunga Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili la Bakiza lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idissa Abdulwakil Mnazi Mmoja  jana Desemba 13, 2018, Balozi Iddi alisema wataalamu wa lugha ya kiswahili wana kazi ya kupunguza changamoto zinazojitokeza katika lugha hiyo hasa  katika matumizi yote.
Balozi Iddi, ailitaka Baraza la Kiswahili Zanzibar {BAKIZA} kuchukuwa jitihada za makusudi  kwa kuandaa maonyesho ya vitabu vya kiswahili vyenye hadhi ya Kimataifa ili wapenzi wa lugha hiyo kutoka  pande zote  za Dunia waweze kufika visiwani humo  kujionea wenyewe na kufaidika na Lugha hiyo adhim ya kiswahili.


 Dk. Shani Omar akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Iddi, kutokana na mchango wake wa kufundisha lugha ya kiswahili.
Balozi Iddi alisema mifumo mingi ya mawasiliano  ikiwemo Mitandao ya Kijamii kama vile Vaiba, Twita, Whatsapp, Imo na mifumo mengine ambayo inakuwa vigumu kuipitia na kuihakiki kwa kuwa haimo katika mfumo wa lugha ya Kiswahili.
Alieleza kwamba Maonyesho ya Vitabu yatasaidia kujenga utamaduni wa watu  kupenda kusoma vitabu kama ilivyoainishwa na wasomi mbali mbali Duniani akitolea mfano nyumba isiyo na vitabu ni sawa na chumba kisicho na dirisha.
Alitahadharisha kwamba Utamaduni huo usipoendelezwa kwa usimamizi wa Wataalamu na wasahili wenyewe  upo uwezekano wa kuwa na Taifa la Vijana wanaotegemea kupata Elimu yao kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa bahati mbaya imetawaliwa zaidi na mambo ya starehe pamoja na uzushi mwingi.
Alisema kitabu kinaweza kuwa ni mshauri na nguzo ya kujitegemea katika kupata maarifa mapya yatakayoongeza umahiri wa mtu ambae akili yake inahitaji matunzo, sawa na bustani inayohitaji kurutubishwa na kupaliliwa ili iweze  kunawiri vyema.

BAADHI ya Wahadhiri wa Vyuo Vikuu mbali mbali Duniani wanaofundisha lugha ya kiswahili wakiwa sehemu ya Wana Kongamano hilo la Pili la Kiswahiuli lililofanyika Visiwani Zanzibar jana wakimsikiliza Balozi Iddi (hayupo pichani)..
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba ni makosa kudhani kuwa kusoma vitabu inawahusu wanafunzi na walimu pekee ambapo baadhi ya wakati wakifikiria ni kopoteza muda.
Alisema Lugha ya Kiswahili kwa sasa tayari inafundishwa ndani ya vyuo vikuu tofauti ulimwenguni ikiwa ni miongoni mwa biashara kubwa ya kimataifa hivyo waswahili wasipokuwa na jitihada ya kuzitafuta fursa zinazozalishwa na kiswahili wanaweza  kubakia nyuma.
Amefafanua  kwamba mataifa mengi ulimwenguni yanahitaji wataalamu wa kiswahili ambapo  vijana wanapaswa  kuamka na  kuichangamkia fursa hiyo muhimu.
Alisisitiza waswahili kukiendeleza, kukienzi na kukitunza kiswahili ili Zanzibar ionekane kweli ndio chimbuko la lugha hiyo  na tayari hivi sasa tayari lugha hiyo inatumika  katika Mikutano ya Kimataifa kama vile Sadc, AU na hata Umoja wa Mataifa.
 Ameipongeza Wizara ya Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Baraza la Kiswahili, Watendaji, Waandaaji wa Kongamano pamoja na Wahadhiri kutoka ndani na nje ya nchi kwa kushiriki mijadala na Maonyesho ya vitabu yaliyosaidia kuimarisha uhimili wa lugha ya kiswahili inayozidi kutanuka ulimwenguni kote.
Akizungumza Katibub Mkuu Wizara  ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar  Omar Hassan Omar aliiomba jamii kuwa na utamaduni wa kusoma, kuandika na kuchapisha vitabu ili kuwapa ufahamu wa lugha waswahili.
Omar alisema katika kulifanikisha hilo aliwataka wataalamu wa Lugha ya kiswahili kuutumia ujumbe wa mwaka huu unaosema kiswahili fahari yetu kwa maendeleo ili kwenda sambamba na azma hiyo muhimu.
Hata hivyo wanakongamano hao wametoa mapendekezo 25 yaliyoainishwa kufuatia majadiliano ya kina yaliyoshirikisha magwiji wa lugha hiyo muhimu inayosimamia na kulinda Utamaduniwa mswahili.
Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na wazo la kuanzishwa kwa mfuko wa Uchapishaji utakaotoa fursa ya kusaidia waandishi wachanga wa Vitabu, Baraza la kiswahili kutangaza kazi zake ndani na nje ya nchi pamoja na uwepo wa siku maalum ya kukumbukwa waandishi wa kiswahili Zanzibar ili Jamii ielewe mchango wa waasisi hao wa lugha.
Azimio jengine muhimu ni lile la kuitaka serikali kuchukuwa hatua kali dhidi ya watu wanaoiba kazi za Waandishi wa vitabu ili kulinusuru soko lao linaloweza kuwapatia tija kutokana na Uandishi huo.

BALOZI Iddi, (kati kati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wahadhiri pamoja na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili la Bakiza lililofanyika Zanzibar kwa mara ya Pili.

Kongamano hilo la kimataifa la s Alilitaka Baraza la Kiswahili {BAKIZA} kuchukuwa jitihada za makusudi kipindi kijacho kwa kuandaa Maonyesho ya Vitabu vya Kiswahili vyenye hadhi ya Kimataifa ili wapenzi wa Lugha hiyo kutoka kila pembe ya Dunia  wafike Zanzibar kujionea wenyewe na kufaidika na Lugha hiyo adhim.
Alilitaka Baraza la Kiswahili (BAKIZA) kuchukuwa jitihada za makusudi kipindi kijacho kwa kuandaa Maonyesho ya Vitabu vya Kiswahili vyenye hadhi ya Kimataifa ili wapenzi wa Lugha hiyo kutoka kila pembe ya Dunia  wafike Zanzibar kujionea wenyewe na kufaidika na Lugha hiyo adhim.
Alilitaka Baraza la Kiswahili {BAKIZA} kuchukuwa jitihada za makusudi kipindi kijacho kwa kuandaa maonyesho ya vitabu vya kiswahili vyenye hadhi ya kimataifa ili wapenzi wa lugha hiyo kutoka kila pembe ya Dunia  wafike Zanzibar kujionea wenyewe na kufaidika na lugha hiyo.
Waliopata zawadi kwa niaba ya wenzao ni Profesa Baby Masamba, Dk  Shani Omar, Profesa Shahal Ahmed, Pacific Malonga, Ala Sala Abdulwakil, Walad Bin Walad, Makoto Promoto, Maseleka, Legele pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA Bibi Mwanahija Ali Juma.

No comments