Breaking News

ASKARI WA KIKE HAKIKISHENI MNAPANDA VYEO KWA JUHUDI ZENUI-SAMIA.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na askari polisi wa kike waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya gwaride la maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,  mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba.


                           Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan leo Januari 11, 2019 ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya Askari Polisi Mfikiwa Chake Chake Pemba.

Makamu wa Rais ambaye yupo Pemba kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Samia aliwataka viongozi wa vikosi kuongeza nguvu na kuhakikisha usimamizi wa shughuli za ujenzi wa makaazi ya askari unakamilika kama ulivyopangwa.


SAMIA, akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba. Leo Januari 11, 2019  (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais).
“Mwaka jana Machi 20, 2018 niliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba za makaazi wa askari wetu, hivyo basi lazima lengo litimie kama tulivyozungumza siku ya uwekaji jiwe la msingi,” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande mwingine Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji, alisema kuwa mipango ya kumalizia ujenzi wa makaazi bora ya askari polisi bado inaendelea na kuahidi kuikamilisha kwani ni dhamira ya jeshi la polisi kuhakikisha askari wake wanaishi sehemu salama.

Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais aliwasalimia askari wa kike waliokuwa kwenye maandalizi ya gwaride maalumu la siku ya maadhimisho ya kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Matakatifu ya Zanzibar yatakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Gombani, Chake Chake Pemba.

 ASKARI Polisi wa kike wakika katika maandalizi ya sherehe za Mapinduzi.

 Hata hivyo, Makamu wa Rais Samia aliwataka askari hao kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao.


Alisema anaamini kuwa askari hao watapanda vyeo kwa jitihada ya kazi zao na si vinginevyo, hivyo waendelee kuchapa kazi kwa kwa bidii sana.

No comments