Breaking News

DK. MWANJELWA AIPONGEZA PTF KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA.


 NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa  akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya  kikazi kutembelea ofisini kwao Jjijini Dar es Salaam  leo Januari 8, 2019.

 
                              Na Mary Mwakapenda

MFUKO wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Uchumi wa Viwanda inayohimizwa na Rais Dk. Pombe Magufuli, kwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, akina mama na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali Jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea watumishi wa mfuko huo.

Ziara hiyo ilikuwa na  lengo la kufahamu majukumu yake na kuhimiza uwajibikaji, ambapo alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Dk. Mary (kushoto), akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji  wakati wa ziara ya  Dk. Mary.Dk. Mwanjelwa alisema kuwa, makundi yaliyopatiwa mikopo ambayo ni kundi maalumu la walemavu la Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha Uwazi Shaloom cha akina mama wasindikaji.

Vingine ni kikundi cha Makini Food Supplis cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda kwa vitendo kwani wanazalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni mvinyo, viungo vya mchuzi, viungo vya chai, siagi ya karanga, mango pickle na begi za wanafunzi wa shule za awali, za msingi na vyuo.

Dk. Mwanjelwa aliongeza kuwa, PTF imejitofautisha na taasisi nyingine za kifedha kwani  inajali makundi maalumu yote kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu na yenye riba ndogo zaidi bila ubaguzi wowote.
ROSE Kalulika (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mary kuhusu bidhaa zinazozalishwa  na kikundi cha akina mama wa kikundi cha Uwazi  Shaloom  wakati wa ziara hiyo. 
 


Kwa upande wake, mwakilishi wa kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), Aneth Gerana alisema wanaishukuru PTF kwa kuwapatia mikopo kwani imekuwa ikiwanufaisha sana ikizingatiwa kwenye benki walikuwa hawadhaminiki, hivyo PTF imekuwa mkombozi kwao.

Aneth alisisitiza kuwa, kupitia mkopo wa fedha wa PTF wao kama walemavu wameweza kuuthibitishia umma kuwa, wanaweza kwa kuzalisha mvinyo wenye ubora.

Pia, alisema wana hakika ya kuifikia ndoto ya kuwa na kiwanda cha mvinyo kikubwa Afrika ya Mashariki ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano.
 WASHIRIKI katika vkundi vya  Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), Uwazi Shaloom,  Makini  Food Supplies na MAB wamkisikiliza Naibu Waziri Mry Mwanjelwa wakati akishuhudia bidhaa wanazo zitengeneza.Mwakilishi huyo aliiomba PTF kuwapatia mafunzo ya kompyuta wao kama kundi maalumu la walemavu ili mafunzo hayo yaweze kuwasaidia kutafuta masoko kwa njia ya mtandao,  ombi ambalo lilitiliwa mkazo na Dk. Mwanjelwa.

Kutokana na ombi hilo, Dk. Mwanjelwa alitaka PTF kuwapatia mikopo ya vifaa vitakayowawezesha kununua kompyuta zitakazowarahisishia  utafutaji wa masoko kwa njia ya mtandao. 

Naye, mwakilishi wa kikundi cha MAB cha vijana wanaotengeneza begi, Amon Philemon alisema mkopo wa PTF umewawezesha kuwa wajasiriamali wa  kutengeneza begi za wanafunzi wa kuanzia shule za awali hadi vyuo vya elimu ya juu.
 NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa (kulia) akiwasisitiza watumishi wa PTF kutoa huduma nzuri  kwa walengwa wa mikopo inayotolewa  na PTF. (Picha zote na James Mwanamyoto-UTUMISHI).Philemon ameainisha kuwa, katika begi wanazozitengeneza, wanaweka picha za wanafunzi husika, majina yao na logo  lengo likiwa ni  kudhibiti wizi shuleni na vyuoni.

Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ni Taasisi ya Kifedha inayotoa mikopo ya fedha na vifaa nchini kwa makundi ya akina mama wajasiriamali wazalishaji, kundi maalumu la watu wenye ulemavu.

Pia, kwa vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi lengwa kabla ya kutoa mikopo kwa wanufaika hao wa PTF.

No comments