Breaking News

OLE WAKE ATAKAEVURUGA AMANI ZANZIBAR-BALOZI IDDI.


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na wananchi walioshiriki kuona mchezo wa Ng’ombe katika Uwanja wa Kiuyu Minungwini, jana Januari 9, 2019. 
                    Na Othman Khamis Ame, Pemba

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba Serikali haitosita kumuweka mahali panapostahiki mtu au kikundi chochote kinachokusudia kuichezea amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar  ya Mwaka 1964.

Alisema zipo tetesi za shari zinazoandaliwa na baadhi ya watu kutaka kuwafitinisha wananchi  dhidi ya Serikali yao, lakini vyombo vya dola kamwe havitakubali kuvumilia vitendo hivyo.

Balozi Iddi,  alitoa onyo hilo jana Januari 9, 2019 wakati akitoa salamu kwenye burdni ya mchezo wa Ngo’ombe uliofanyika Kiuyu Minungwini Mkoa Kaskazini Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
BAADHI ya viongozi na wananchi wakiangalia burdani ya mchezo wa Ng’ombe katika Uwanja wa  Kiuyu, Minungwini ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za Maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Alisema mkorofi yeyote atakayeamua kujiingiza katika mtego wa watu hao wanaohisi kwamba Zanzibar haifanani na nchi  zilizovurugika  amani,  ajaribu kama hakukiona cha mtema kuni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, aliikumbusha Jamii kuendelea kulinda amani  ya Taifa itakayosaidia kuimarisha sambamba na kuendeleza michezo hapa nchini.

 NG’OMBE aitwae Kivumbi akitimua vumbi kama jina lake wakati akichezwa kwenye Burdani ya Ng’ombe uwanjani wa Kiuyu, Minungwini mkoa  wa Kaskazini Pemba.Aliwapongeza wananchi wa Kiuyu Minungwini kutokana na juhudi zao za kuendeleza mchezo wa Ng;ombe ambao ni maarufu na wa asili kwa miaka mingi katika historia ya Kisiwa cha Pemba.

Balozi Iddi, alisema Burdani ya mchezo wa Ng’ombe imezoeleka katika Mataifa mengi ya Ulaya hasa Spain ambao umepata umaarufu mkubwa kwa wadau wa michezo.


 MCHEZAJI mahiri wa mchezo wa Ng’ombe akimkwepa Ng’ombe Toba Rohoyangu wakati wa burdani ya mchezo huo ulioshuhudiwa na mamia ya wan anchi wa mikoa miwili ya Pemba.Burdani hiyo ya aia yake iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi wa  wilaya tofauti za Kisiwa cha Pemba ilihusisha Ng’ombe waliopewa majina ya Kivumbi, Kiburugo, Toba Rohoyangu pamoja na Kaza roho.

Mapema, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Mohamed Aboud Mohamed, alisema burdani ya mchezo wa Ng’ombe ni miongoni mwa michezo iliyojumuishwa ndani ya Sera ya Serikali kupitia Wizara inayosimamia Michezo kudumisha mila na utamaduni wa Mzanzibari.

 NG’OMBE  Kaza Roho akikimbizana na wacheza Ng’ombe kwenye burdani ya mchezo huo. (Picha zote na – OMPR – ZNZ.).Waziri Mohamed, alisema wananchi wa Zanzibar wamekuwa shuhuda wa maendeleo makubwa katika sekta ya michezo yaliyofikiwa Zanzibar ndani ya kipindi cha miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

No comments