Breaking News

SAMIA ASIFU CONGO KUBADILISHANA MADARAKA KWA AMANI. MAKAMU wa Rais  Samia Suluhu Hassan, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika Uwanja Mkuu wa Michezo mjini Kinshasa, wengine pichani ni Rais Felix Tshisekedi pamoja na Joseph Kabila. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
                            Na Mwandishi Wetu, Congo
MAKAMU wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na amani.
Alisema ana imani kuwa viongozi wan chi hiyo wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.
Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli, aliyasema hayo leo Januari 25, 2019 mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi.
“Linalofurahisha ni kwamba, hii  ni mara ya kwanza kwa Nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa,” alisema Makamu wa Rais.
 Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Felix Tshisekedi alipata takribani kura Milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura Milioni 6.4, Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata Uhuru wake kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na utulivu.MAKAMU wa Rais  Samia Suluhu Hassan, akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (hayupo pichani), katika Uwanja Mkuu wa Michezo mjini Kinshasa

No comments