Breaking News

JERRY MURO AISHUKIA VIKALI YANGA, AWANYOOSHEA VIDOLE VIONGOZI NA WACHEZAJI.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga, Jerry Murro amewajia juu Wanayanga kwa kusema kuwa wao ni sababu ya kushuka kwa morali na ufanisi wa timu hiyo nje na ndani ya uwanja.

Murro ameyasema hayo jana mara baada ya mchezo wa Simba na African Lyon kukamilika katika dimba la Shekh Amri Abeid Jijini Arusha  kwa Simba kuibuka na ushindi  wa bao 3-0.

Amesema mpira wa sasa unahitaji ufanisi mkubwa jambo ambalo linapaswa kufanywa na kila aliye kwenye nafasi ya kuisaidia timu wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Viongozi wa timu, lakini anashangazwa  kitendo hicho hakifanyiki ndani ya klabu yake ya Yanga.

KUHUSU UONGOZI.
Murro amezungumzia nafas ya usemaji ambapo amesema alipoondoka Yanga alitegemea kuona nafasi aliyo iacha ingefanya makubwa kuliko aliyo yafanya yeye lakini imekuwa kinyume na matarajio yake.

“Sitaki kumuongelea msemaji wetu, lakini kiukweli Yanga imepooza, nilitegemea viatu vyangu vingembana angefanya mambo makubwa zaidi niliyo yafanya lakini badala yake karudisha morali ya klabu kuwa ziro.” Amesema Murro.

KUHUSU WACHEZAJI.
Murro  amesema kuna baadhi ya wachezaji hawakustahili kuwepo ndani ya Klabu ya Yanga kwa sababu mbali mbali alizo ziainisha.

“Sio kama namchukia ila Ngasa amesha cheza Yanga miaka na miaka, ingefaa aangalie kazi nyingine ya kufanya sio kurudi Yanga kama mchezaji, akajifunze ukocha aje kuwa hata kocha wa vijana.” Amesema Murro.

“Haya Boban yupo pale, anatafuta nini yulee..! Mwili wake umechoka, maisha yake yamechoka,akili imechoka kwani anatafuta nii pale..!?” amehoji Murro.

KUHUSU KOCHA
Murro amedai kuwa Yanga kwa sasa haina mwalimu mzuri wa kufundisha mpira badala yake ina muhamasishaji tuu.

“ Mwalimu hajuwi wachezaji, Yule ni mhamasishaji ambaye anatosha kutusaidia kuchangisha fedha lakini kimpira Zahera sio mwalimu wa Mpira.” Amesisitiza Murro.

Kwa upande wake Msemaji wa Simba Haji Manara amesema kwa sasa hana mpinzani katika tasnia ya usemaji wa klabu nchini sababu aliyekuwa anashindana nae kwenye nafasi hiyo Jerry Murro kuwa na majukumu mengine ya kiserikali.

No comments