Breaking News

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WASANII.

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu katika matukio mbalimbali akizungumza na wasanii kwenye kongamano la wasanii Tanzania kuhusu athari za matumizi na biashara ya dawa za kulevya lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akiongoza viongozi wa meza kuu na wasanii kusimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop Tanzania Golden Jacob Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo kabla ya kuanza kuhutubia 

Wasanii wa Filamu na Muziki wakiwa wamesimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop  Golden Jacob Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akihutubia wasanii wa fani mbali mbali.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akiangalia kwa umakini Sanaa ya maigizo iliyokuwa ikionyeshwa na wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliokuwa wakionyesha madhara ya dawa ya kulevya.


No comments