Breaking News

PICHA : MAKAMU WA RAIS AWASILI SHINYANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa kata ya Tinde waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili mkoani Shinyanga akitokea mkoani Tabora.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua  kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI  Mwita Waitara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments