Breaking News

PICHA : ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KALIUA NA URAMBO MKOANI TABORAPicha ya Jengo la Upasuaji lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na michango ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alipokuwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo wilayani Kaliua, Tabora.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua, Tabora. 

Picha iliyopigwa kutoka juu ikionyesha wananchi walivyojitokeza kwa wingi kwenye mkutano ambao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alikuwa mgeni rasmi. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa zaidi ya pikipiki 15 kwa vijana wa boda boda ikiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akikabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 250 kwa vikundi 61 vya ujasiriamali ukiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora.

Sehemu ya wakazi wa Usoke Mlimani walioihudhuria mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, Urambo mkoani Tabora. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipokea kitabu cha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo la Urambo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Margaret Sitta mara baada ya kuhutubia katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Usoke Mlimani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akisomewa taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Kaliua na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua John  Pima .(Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments