Breaking News

PICHA: ZIARA YA MAKAMU WA RAIS NZEGA NA UYUI MKOANI TABORA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Hussein Bashe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata gesi, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia).
Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Tabora. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara,  Mbunge wa Igalula Mussa Ntimizi (kulia) na Mkuu Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya (kushoto) mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Igalula, wilayani Uyui mkoa wa Tabora. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akimpa mkono wa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mtoto wake mdogo wa kiume Zul muda mfupi kabla ya mazishi Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akimpa mkono wa pole  JR Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mdogo wake Zul, kulia ni Baba wa Marehemu Zul, Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla muda mfupi kabla ya mazishi yaliofanyika Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments