Breaking News

PICHA : ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI IRAMBA – SINGIDA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba (kulia) mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. 


Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge Mwigulu Nchemba.


Makamu wa Rais Samia Suluhu akihutubia mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida.


Makamu wa Rais Samia Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Maulid Njau (kushoto) juu ya maboresho na ukarabati wa chuo cha ualimu Kinampanda, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais).

No comments