Breaking News

PICHA:WAZIRI JENISTA MHAGAMA AKIKAGUA MIRADI YA VIJANA SONGWE.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)  Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika kupitia kituo cha maendelo ya vijana, Sasanda alipotembelea kuona mradi walioanzisha katika Kata ya Nyimbili. (Mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela.

Waziri Jenista Mhagama akizungumza na vijana wanaopata mafunzo ya kilimo bora na ufugaji wa kisasa katika kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe alipofanya ziara kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akimwagilia maji mti alioupanda katika kituo hiko cha Sasanda alipofanya ziara katika kituo hicho kukagua maendeleo na miradi ya vijana. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bi.  Tusubileghe Benjamin na (Kulia) ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.

 
Bw. Zawadi Mdolo akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu mafunzo wanayopatiwa katika shamba darasa juu ya kulima bora na upatikanaji mazao mengi. (Mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa na kupata maelezo ya vifaa vinavyotumiwa na vijana wa kituo cha Sasanda katika shughuli ya kuvua samaki.

Lusekelo Mbukwa akimueleza jambo Waziri Jenista Mhagama kuhusu majani wanayotumia kwa ajili ya malisho ya ng’ombe yanayosaidia ukuaji bora wa mifugo hiyo na upatikanaji wa maziwa mengi.

Oliveta Mwashilindi akimueleza jambo Waziri Jenista Mhagama kuhusu bidhaa ya asali inayotengenezwa na kikundi cha vijana cha Maisha Daily kilichopata mafunzo ya ufugaji nyuki katika kituo cha Sasanda.


Waziri Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Rasupashoma Group, Ibrahim Malabela jinsi wanavyotengeneza viatu bora na vyenye kudumu kwa muda mrefu. (Mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela na (Kulia) niMkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.

Waziri Jenista Mhagama akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo cha Sasanda.

Muonekano wa shamba darasa moja wapo lililopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda Mkoani Songwe.(Picha zote na Ofisi ya Waziri MkuuKazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu)


No comments