Breaking News

RAIS MAGUFULI APIGA HODI MWAISELA KUJUA HALI YA MBUGE.Na Mwandishi Wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Februari, 2019 amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika wodi ya Mwaisela ndani ya  Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.


Mhe. Kitwanga alilazwa hospitalini hapo tangu tarehe 31 Januari, 2019 baada ya kupata ajali iliyopelekea kuhitaji huduma ya haraka.

Akiwa wodini hapo Rais Magufuli ameshiriki sala ya pamoja ya kumuombea Kitwanga apone haraka na kurejea kwenye majukumu ya kujenga Taifa,pia alichukua fulsa hiyo  kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuwahudumia wagonjwa.Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mhe. Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofika hospitalini hapo na huenda akapona mapema zaidi tofauti na hapo mwanzoni walivyodhani.

No comments