Breaking News

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYA YA SIKONGE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Sikonge ambaye pia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda(kulia) mara baada ya kuwasili Sikonge mkoani Tabora ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akimwagilia mei wa kumbukumbu alioupanda mara baada ya kuweka  jiwe la msingi  la ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora. 

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda akihutubia wananchi katika uwanja wa TASAF Sikonge mkoani Tabora.

8: Sehemu ya Wananchi wa Sikonge, mkoani Tabora waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

9:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya TASAF wilayani Sikonge mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akizungumza na viongozi wa vikundi vya ujasiriamali ambayo vimekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 40 kama sehemu ya 10%ya mapato ya Halmashauri ambapo vikundi 11 vimefaidika na mkopo huo.(Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)


No comments