Breaking News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU ILIPOTUA JNIA


Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Paul Rwegwasha akitoa taarifa fupi ya Mamlaka kuhusu mpango wa  usimamizi na uendeshaji jengo la III la abiria kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu  ambaye ni Mbunge wa Kasulu mjini Daniel Nsanzugwako (mwenye kofia) akiuliza swali mara baada ya kusomwa taarifa ya mradi wa Jengo la III la abiria wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa  akijibu hoja maswali mbalimbali ya kisera kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa akijibu maswali kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo aliekaa kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso.Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.


Mhandisi Burton Komba kutoka Wakala wa Barabara akitoa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la III la abiria kwa Wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara katika Jengo hilo mapema leo.

No comments