Breaking News

MAJALIWA KATIKA KIKAO CHA UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO WA BAJETI YA MWAKA 2019/2020 BUNGENI MJINI DODOMA.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma Machi 12, 2019. Mheshimiwa Majaliwa amekwenda Bungeni kuhudhuria kikao cha Uwasilishwaji wa Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020; na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha Uwasilishwaji wa Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020; na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020,  Bungeni jijini Dodoma, kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na kulia ni Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai.

Waziri wa Fedha Philip Mpango akiwasilisha Mpango na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020; na Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments