Breaking News

MAKAMU WA RAIS AWASILI UGANDA KUSHIRIKI MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019.

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda. 

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Aziz Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda. 

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

No comments