Breaking News

PICHA: ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI KAHAMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. 

Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka .

Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72. 

Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kata ya Isagehe mara baada ya kukagua  matanki mawili ya maji
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa, wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Rebecca Stephen.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakicheza ngoma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa  Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa la mradi wa TEA na P4R. Mkamu wa Rais yupo wilayani Kahama kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za maendeleo.(Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments