Breaking News

PICHA:KAMATI YA KUDUMU YA MADINI YA BUNGE ILIVYO TEMBELEA MRADI WA UMEME NJOMBE.

Moja ya nguzo, kati ya nguzo 711 (Tower erection) inayosafirisha umeme wa msongo wa kV 220 kutoka Makambako hadi Songea iliyojengwa kupitia mradi wa umeme wa Makambako- Songea.

Baadhi ya mitambo ya umeme katika kituo cha kupoza umeme cha Makambako mkoani Njombe ambacho kimejengwa kupitia mradi wa umeme wa Makambako- Songea.


Waziri wa Nishati, Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutembelea kituo cha kupoza umeme cha Makambako mkoani Njombe. Wa Pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariamu Ditopile Mzuzuri na Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati walipotembelea kituo cha kupoza umeme cha Makambako mkoani Njombe. Wa Pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariamu Ditopile Mzuzuri.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu kituo cha kupoza umeme cha Songea ambacho kimejengwa kupitia mradi wa umeme wa Makambako-Songea. Wa Pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariamu Ditopile Mzuzuri.

No comments