Breaking News

PICHA:MATUKIO MBALIMBALI YAKIONYESHA MAANDALIZI YA MRADI WA UMEME RUFIJI


Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Tito Mwinuka (katikati) wakikagua eneo kutakapotekelezwa mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115), wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula (katikati), Waziri wa Nishati, Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Gulamali (wa Pili kulia) wakimsikiliza mtaalam kutoka kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy Electric wakati akizungumzia mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115).

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, pamoja na Waziri wa Nishati, Medard Kalemani (wa nne kutoka mbele) wakiwa  katika eneo ambalo litatumika kutekeleza mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115) mara baada ya kufanya  ziara katika eneo la mradi huo.

Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akiwaongoza baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mara walipofika katika eneo kutakapotekelezwa mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115), wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani, (katikati), akizungumza na Wataalam wanaosimamia na wanaotekeleza mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115) mara baada ya kufika katika eneo la mradi huo akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Moja ya nyumba inayojengwa na mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme wa Rufiji ambapo katika eneo hilo kunajengwa  kambi ya muda ya Wafanyakazi wa mradi huo.


No comments